Kiswahili · Kidato 1

Mada kuu ya tano

Dakika 2 za kusoma ·

Yaliyomo

Usimulizi Wa Hadithi

Usimulizi ni nini? Ni kuelezea mtu au watu jambo fulani ambalo limetokea katika muda uliopita , hivi karibuni, au zamani sana.Kutokana na fasili hiyo , tunapata aina mbili za usimulizi

  • USIMULIZI WA HADITHI; Hadithi ni maelezo ya moja kwa moja ambayo yanahusu visa vinavyorithishwa kutoka zamani, visa hivyo vinaweza kuwa halisi au vya kubuni.

Dhima au kazi za hadithi

  • Kuelimisha
  • Kuonya
  • Kukuza ujasiri
  • Kukuza utamaduni
  • Kuchochea fikra za kijasiri
  • Kukuza uhusiano
  • Kukuza ufahamu wa lugha

Mbinu za usimulizi wa hadithi

  • Kujua muundo wa hadithi. Mfano;
  • Mwanzo, Hadithi hadithi……………
  • Kati, Hapo zamani za kale…………
  • Mwisho, Hadithi yangu ikaishia hapo.
  • Kujua mbinu za kisanaa za usimulizi .Mbinu hizo ni
  • Uigizaji; Ni kuiga au kuigiza sauti, matendo, miondoko au mavazi ya wanavyosimulia.
  • Michepuko; Hii ni namna ya kuacha kwanza kusimulia hadithi moja kwa moja na kuanza kuangalia mambo mengine kwa ufupi.
  • Utumiaji wa lugha
  • Kushirikisha hadhira. Mfano; kuiuliza hadhira maswali, kuiimbisha hadhira nk.
  • Uzingatiaji wa sauti, sauti isiwe juu sana au chini sana, au chini sana lakini iwe yenye kusikika vizuri.
  • USIMULIZI WA HABARI( Nini maana ya habari?); Ni taarifa za kweli kuhusu mambo ya kweli .myanayotokea katika jamii na wala si mambo ya kubuni.AU ni namna ya kumwelezea mtu kuhusu jambo fulani ambalo limetokea au limewahi kutokea wakati fulani.

Misingi Ya Usimulizi Wa Habari

  • Kutumia sauti inayosikika.
  • Kutumia lugha fasaha na inayoendana na tukio linalosimuliwa.
  • Kuzingatia muundo wa usimulizi yaani, utangulizi, kiini na mwisho.
  • Ubainishaji wa habari kwa kuzingatia mahali pa tukio, muda wa tukio na athari za tukio.
  • Uhusiano kati ya msimuliaji na msikilizaji, Mfano; umri na jinsia.
  • Muktadha wa tukio.

MASWALI.

1.Habari ni nini?

2.Eleza dhima za usimulii wa hadithi katika jamii yako.

3.Usimulizi wa habari na wa hadithi, kwa kawaida huhusisha pande kuu mbili.Zitaje.

4.Unapowasimulia watu habari unatakiwa kutumia mbinu zipi ili wasikilizaji waweze kukusikiliza bila kuchoka?

5.Andika habari fupi yoyote iliyowahi kutokea katika jamii yako.

Jaribu quiz ya KiswahiliMaswali 45