Mada kuu ya nane
Dakika 2 za kusoma ·
Ufahamu
Maana ya ufahamu; Ni kipengele katika taaluma ya lugha ambacho humpa msomaji au msikilizaji mbinu za kuelewa kitu alichokisoma au kusikiliza.
Dhima au kazi ya ufahamu
- Kuokoa muda.
- Kuokoa gharama.
- Kuelimisha.
Mambo ya kuzingatia katika ufahamu
- Uzingatiaji wa habari kwa makini.
- Kutambua mawazo makuu na
- Kuelewa vipengele anuai vya kifani kwa jambo linalounda kazi hiyo.
Aina Za Ufahamu
A: Ufahamu wa kusikiliza; Ni ufahamu unaotokana na kusikiliza jambo linaloelezewa na mtu mwingine ana kwa ana au kwa njia ya redio, runinga nk. Usikivu mzuri ndiyo utamwezesha msikilizaji kupata uelewa wa kutosha juu ya yale anaypyasikiliza.
Mbinu za kujibu maswali yatokanayo na habari ya kusikiliza
- Kuvuta umakini na kusikiliza bila kuruhusu kuingiliwa na mawazo mengine.
- Kusikiliza habari yote kwa makini.
- Kusikiliza kila swali kwa makini .
- Kutafakari kwa makini.
- Kujibu kila swali kwa ufupi na usahihi.
Dhana Ya Ufupisho
Maana ya ufupisho; Ni kueleza jambo kwa maneno machache bila kupoteza maana yake ya msingi .
Dhima au kazi au faida ya ufupisho
- Kuokoa muda.
- Kuokoa gharama, Mfano katika simu.
Dhana Ya Usomaji
Aina za usomaji;
- Usomaji wa haraka; Hutumiwa kuimarisha kasi ya ,msomaji kwa kutumia muda maalumu uliotengwa na kiasi maalumu cha maneno . Mfano; usomaji wa magazeti, vitabu vya hadithi nk.
- Usomaji wa taratibu na kwa makini; Usomaji huu hutumia muda mrefu, ukimruhusu msomaji kuchunguza mambo mengi katika yale asomayo.
- Kusoma kwa sauti; Aina hii ya usomaji hufuata kanuni za usomaji kwa sauti ambazo ni matamshi,viimbo, lafudhi na vituo.
- Matamshi; Ni namna maneno yanavyosemwa kwa mdomo wa msomaji. Kila neno linatakiwa litamkwe kwa usahihi, vinginevyo litatoa maana tofauti. Mfano zua badala ya jua,maralia badala ya malaria .
- Kiimbo; Ni kupanda na kushuka kwa sauti katika uzungumzaji au usomaji. Kiimbo huondoa utata katika baaadhi ya maneno kama vile; barabara na barabara.
- Vituo; Msomaji anatakiwa kusoma kwa kuzingatia alama za vituo katika kila sentensi. Vituo vinaweza kuwa nukta, viulizi, au mshangao .
- Kusoma kimya; Ni kusoma bila kutamka maneno kwa sauti inayosikika.
Faida za kusoma kimya
- Hupata nafasi ya kupima mwendo wa msomaji na kiasi cha uelewa.
- Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine.
- Hukwepa kuzingatia kanuni za matamshi na
- Huweza kusoma maandishi mengi kuliko kusoma kwa sauti.
Mambo ya kuzingatia katia usomaji
- Ufahamu wa lugha.
- Ubainishaji wa mawazo makuu.
- Kusoma kwa burudani; Ni aina ya usomaji ambao msomaji husoma kwa ajili ya kujiburudisha.
Maswali
1.Nini maana ya ufahamu?
2.Ufahamu una umuhimu gani katika katika usomgik3
aji wa darasani?
3.Eleza taratibu ambazo msomaji wa kitabu anatakiwa kuzifuata anaposoma kitabu kimya.
4.Eleza mambo muhimu ambayo msikilizaji wa habari au hadithi anatakiwa kuzingatia anaposikiliza hadithi au habari ili apate kuielewa vizuri habari au hadithi hiyo.
5.Taja vipengele muhimu vya kuchunguza zaidi wakati wa kusoma kitabu.
