Kiswahili · Kidato 2

Uundaji wa maneno

Dakika 7 za kusoma ·

Yaliyomo

Uundaji Wa Manemo

Correction: the heading must be correct.

Uundaji Wa Maneno

Uundaji wa maneno mapya ni uzalishaji au kuzalisha maneno mapya.

Njia hii huiwezesha lugha kukidhi mahitaji ya mawasiliano.

Njia Za Uundaji Wa Maneno

Uambishaji

Uambishaji ni upachikaji wa mofimu katika mzizi wa neno.

Mofimu zinazopachikwa katika mizizi ya maneno huitwa viambishi.

Uambishaji haufanywi kwa kubahatisha tu. Huzingatia kanuni fulani na huhusisha aina mbalimbali za maneno kama ifuatavyo.

  1. Uambishaji wa nomino:

Uambishaji huu hutokea viambishi vinapopachikwa kabla au baada ya mzizi wa neno. Mfano

  • M-gonjwa (kabla ya mzizi)
  • Wa-ganga (kabla ya mzizi)
  • Pig-o (baada ya mzizi)
  • Makaribisho (kabla na baada ya mzizi)
  1. Uambishaji wa vitenzi:

Hutokea katika mzizi wa kitenzi. Hutokea kabla au baada ya mzizi. Mfano

  • Wa-li-tib-iw-a
  • Ha-ji-king-i
  • Si-ja-l-a-zw-a
  1. Uambishaji wa viwakilishi:

Viwakilishi fulani huundwa kwa kupachikwa viambishi kabla au baada ya mzizi. Mfano

  • Yu-le
  • Ku-le
  • Yo-yo-te
  1. Uambishaji wa vielezi:

Mfano

  • M-toto
  • Ki-toto
  • U-puuzi
  • Ki-puuzi
  1. Uambishaji wa viunganishi:

Viambishi mbalimbali hupachikwa kabla ya mzizi [a] ili kuunda kiunganishi. Mfano

  • Kiunganishi Wa-, kiambishi w-a-. Mfano: Mtoto / watoto w-a kaka
  • Kiunganishi La-, kiambishi l-a-. Mfano: Jumba l-a starehe
  • Kiunganishi Pa-, kiambishi p-a-. Mfano: Mahali p-a kupasulia
  • Kiunganishi Kwa-, kiambishi kw-a-. Mfano: Ofisini kw-a daktari
  • Kiunganishi Vya-, kiambishi vy-a-. Mfano: Viatu vy-a Ali

Aina Za Uambishaji

Kuna aina tatu za uambishaji

  • Uambishaji awali
  • Uambishaji kati
  • Uambishaji tamati au mwisho

Uambishaji awali

Ni uambishaji wa viambishi mbalimbali kabla ya mzizi wa neno.

Uambishaji awali hudhihirika zaidi katika nomino na vitenzi.

Uambishaji awali katika nomino hufanya kazi kama vile kuonyesha ngeli. Mfano

  • Kiongozi: Ki-ongoz-i, Vi-ongoz-i (ngeli ya Ki-Vi)
  • Kujiongoza: Ku-ji-ongoz-a (ngeli ya Ku)

Uambishaji awali katika vitenzi

Viambishi hivi ni vya namna mbalimbali na hufanya kazi tofautitofauti kama ifuatavyo.

Viambishi awali vya nafsi au vya kuonyesha ngeli katika umoja na wingi. Mfano

  • a-ta-tes-ek-a, wa-ta-tes-ek-a (ngeli ya Yu-A-Wa)
  • li-me-amk-a, ya-me-amk-a (ngeli ya Li-Ya)

Viambishi vya kukanusha. Mfano

  • Ha-ta-kuj-a
  • Si-ku-amk-a

Viambishi vya njeo au wakati. Mfano

  • A-ta-kuj-a (wakati ujao)
  • Wa-li-chez-a (wakati uliopita)
  • A-na-kul-a (wakati uliopo)

Viambishi vya kuonyesha hali. Mfano

  • A-ki-j-a
  • A-nge-kuj-a

Viambishi rejeshi vya mtenda au mtendwa. Mfano

  • Ni-me-ji-kat-a
  • A-li-ye-kuj-a

Uambishaji kati

Ni uambishaji wa kupachika kiambishi ndani ya mzizi wa neno.

Viambishi vinavyopachikwa huitwa viambishi kati.

Aina hii ya uambishaji haitokei sana katika lugha ya Kiswahili. Mfano: chezw-a, kamatw-a

Uambishaji tamati au mwisho

Huu ni uambishaji wa kupachika viambishi mwishoni mwa nomino.

Nomino zinapopachikwa viambishi hivi, hubadilika na kuwa vielezi. Mfano

  • Nyumba (N) + ni = Nyumbani (E)
  • Mlima (N) + ni = Mlimani (E)
  • Mwaka (N) + ni = Mwakani (E)

Aina Za Viambishi

Kuna aina kuu mbili za viambishi: viambishi awali na viambishi tamati.

Viambishi awali

Hivi ni viambishi vinavyotokea kabla ya mzizi wa kitenzi. Mfano: a-na-chez-a

Dhima au kazi za viambishi awali

  • Kuonyesha nafsi.
  • Kuonyesha idadi ya umoja au wingi.
  • Kuonyesha wakati au njeo.
  • Kuonyesha uyakinishi au ukanushi katika vitenzi.

Viambishi tamati

Ni viambishi vinavyotokea baada ya kiini cha kitenzi. Mfano: Analim-a

Dhima au kazi za viambishi tamati

  • Kukamilisha maana ya neno.
  • Kuzalisha maneno mapya. Mfano: Wanalima, Wanalimia

Mnyumbuliko

Mnyumbuliko ni upachikaji wa mofimu baada ya mzizi wa neno.

Katika dhana ya lugha, mnyumbuliko ni namna ya kuunda neno jipya kwa kutumia neno la awali kwa njia ya kulirefusha zaidi. Mfano:

  • Habari: Habarisha
  • Kata: Katiana
  • Cheza: Chezeana

Dhima au kazi ya mnyumbuliko

  • Hurefusha maneno.
  • Husababisha kutokea kwa maneno mengi, hivyo kupanua msamiati wa Kiswahili.
  • Hupanua maana ya maneno.
  • Huzalisha kauli mbalimbali. Mfano: kutenda, kutendwa, kutendeana n.k.

Aina za mnyumbuliko

Mnyumbuliko wa tendana

Uundaji wa maneno kwa kutumia kauli tendana hufanikiwa kwa kupachika mofimu {an} baada ya mzizi wa kitenzi. Mfano:

  • Ping-a, Ping-an-a
  • Tegeme-a, Tegeme-an-a

Aghalabu, mofimu {ian} hupachikwa katika mzizi. Mizizi ya aina hii huwa na asili ya maneno ya kigeni. Mfano:

  • Hukumu, Hukum-ian-a
  • Heshimu, Heshim-ian-a n.k.

Mnyumbuliko wa tendwa

Viambishi hupachikwa tamati baada ya mzizi wa kitenzi. Mfano

  • Shinda, Shind-w-a
  • Kimbia, Kimbi-w-a

Vitenzi katika kauli tendwa huonyesha tendo lililokusudiwa kumpata mpokeaji. Mfano: Chelsea wamefungwa na Barcelona.

Njia ya kauli

Hii ni namna nyingine inayotumika kuunda maneno.

Kauli tendeka

Ili kuunda maneno kwa kutumia kauli tendeka, tunapaswa kuambatanisha moja ya mofimu zifuatazo kwenye mzizi wa neno: ik, ek, lik na lek.

  • Iwapo mzizi una irabu a, e, i au u, inabidi kupachika mofimu ik. Mfano: Vuta, Vut-ik-a; Panga, Pang-ik-a; Shinda, Shind-ik-a
  • Iwapo mzizi wa neno una irabu e na o, tunapaswa kuambatisha mofimu ek. Mfano: Bonda, Bond-ek-a; Tenda, Tend-ek-a
  • Wakati mwingine inabidi kuambatisha mofimu k. Hii hutokea katika maneno kama yafuatayo: Epu-a, epu-k-a; Ibu-a, ibu-k-a; Inu-a, inu-k-a
  • Mofimu lik hupachikwa ikiwa mzizi wa neno una irabu mbili za a, i au u mwishoni. Mfano: Za-a, zalik-a; Ka-a, kalik-a; U-a, ulik-a
  • Itokeapo kuwa mzizi wa neno una irabu e na o na irabu mbili mwishoni, mofimu lek hupachikwa. Mfano: Zo-a, zolek-a; Ng'o-a, zolek-a

Maneno katika kauli tendeka huundwa kuonyesha maana zifuatazo

  • Kuwa vitendo vimetokea. Mfano: Nyoka ametoka shimoni.
  • Kuwa kitendo kina uwezekano wa kutokea au kutendeka. Mfano: Maziwa yaliyomwagika yatazoleka.
  • Kuwa tendo limetokea kwa ufanisi mkubwa. Mfano: Hotuba imewasilishika; Mtoto wa watu ameumbwa, ameumbika.

Kauli tendesha

Kauli hii hutegemea matumizi ya mofimu yenye maumbo yafuatayo.

Mofimu z. Mfano

  • To-a, to-z-a
  • O-a, o-z-a
  • Ku-a, ku-z-a

Mofimu sh. Mfano

  • Vu-a, vu-sh-a
  • Va-a, vali-sh-a

Mofimu esh. Mfano

  • Ot-a, ote-sh-a
  • Wez-a, wez-esh-a

Mofimu ish. Mfano

  • It-a, it-ish-a
  • Kul-a, l-ish-a

Mofimu ez. Mfano

  • Pend-a, pend-ez-a
  • Wek-a, wek-ez-a

Mofimu fy, vy na y. Mfano

  • Ogo-p-a, ogo-fy-a
  • Le-w-a, le-vy-a
  • On-a, on-y-a

Kauli tendesha huonyesha kuwa tendo limesababishwa na mtu au kitu fulani.

Mofimu

Maana ya mofimu

Mofimu ni neno au sehemu ya neno inayobeba maana maalumu kisarufi, ambayo ikigawanywa katika vipande zaidi hupoteza maana. Mfano: mama, baba, kaka n.k.

Katika mazingira fulani, sehemu ya neno huweza kubeba maana kisarufi. Mfano: Hu-m-pig-a

  • Hu (kuonyesha hali)
  • M (kuonyesha idadi)
  • pig (mzizi wa neno)
  • a (kiambishi tamati)

Aina Za Mofimu

Mofimu huru

Ni aina ya mofimu ambazo zinaweza kusimama zenyewe na kuleta maana.

Mofimu huru haiwezi kuvunjwavunjwa katika vipashio vidogo zaidi na kuleta maana.

Mofimu tegemezi

Ni sehemu ndogo za maneno zenye maana kisarufi.

Mofimu tegemezi haiwezi kusimama peke yake.

Maana ya mofimu tegemezi hujitokeza zinapopachikwa katika mzizi wa neno.

Kuunda Maneno Kwa Kutumia Mofimu

Uundaji wa maneno mengi katika Kiswahili hutokana na uunganishaji wa mofimu mbalimbali. Maneno ya aina mbalimbali yanaweza kuundwa kwa kutumia mofimu mbalimbali kama ifuatavyo.

  1. Kutunga nomino:

Mfano

  • M-geni – wa-geni
  • Ki-kapu – vi-kapu

Hapa mofimu huwekwa kabla ya mzizi ili kubainisha ngeli ya idadi.

Njia nyingine za kutunga nomino ni hizi

  • Kuweka mofimu kabla ya mzizi ili kubainisha udogo au ukubwa. Mfano: ji-tu, ji-ji, ju-mba, ki-kapu nk.
  • Kuweka mofimu kabla ya mzizi ili kubainisha au kupata nomino zenye maana tofauti. Mfano: u-tu, u-huru, u-ganga, u-safiri nk.
  • Kuweka mofimu baada ya mzizi. Mfano: som-o, pend-o, ker-o, leng-o nk.
  • Kuweka mofimu kabla na baada ya mzizi. Mfano: m-pish-i, u-sem-i nk.
  • Kuunganisha mofimu. Mfano: askarikanzu, nusu kaputi, bata maji nk.
  1. Kuunda baadhi ya vivumishi:

Inawezekana kuunda vivumishi kwa kuweka mofimu kabla ya mizizi ya maneno.

Mfano: m-zuri, m-bovu, ki-bovu nk.

  1. Kuunda baadhi ya viwakilishi:

Viwakilishi huundwa kwa kuunganisha mofimu tegemezi.

Mfano: yu-le, wa-le, ku-le, li-pi nk.

  1. Kuunda vielezi:

Mfano: vi-baya, ki-toto, ki-swahili, ki-jinga nk.

  1. Kuunda vihusishi:

Mfano: mw-a, p-a, kw-a, ch-a nk.

  1. Kuunda vitenzi:

Mfano: wa-me-wasili-an-a nk.

Kubainisha Mofimu Katika Maneno

Ili kubainisha mofimu, tunahitaji kuzingatia mambo yafuatayo

  • Kutambua aina ya neno husika.
  • Kuainisha mofimu ili kutenga mofimu huru na mofimu tegemezi.
  • Kutambua maumbo na nafasi ya mzizi.
  • Kupambanua maana ya dhima ya kila mofimu.

Kwa ufupi, maneno mbalimbali yanayoundwa kwa njia mbalimbali hutumika kukidhi mawasiliano miongoni mwa wanajamii wa kada tofauti.

Mfano: wakulima, wafanyabiashara, wanasiasa, wahunzi nk.

Maswali

  1. Nini tofauti kati ya kuainisha na kubainisha?
  1. Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo:

(a) Watapika

(b) Watatapika

(c) Msomaji

  1. Eleza kwa msaada wa mifano manufaa na maana ya neno mnyumbuliko.
  1. Tunga sentensi moja kwa kila neno:

(a) Zikwa

(b) Fupisha

(c) Limika

  1. Fafanua maana na tofauti baina ya mofimu huru na mofimu tegemezi huku ukitoa mifano.
  1. Pachika mofimu ipasavyo katika maneno yafuatayo ili kuunda maneno mengine mawili kwa kila neno:

(a) Kufa

(b) Andika

(c) Soma

  1. Eleza maana ya uambishaji.
Jaribu quiz ya KiswahiliMaswali 39