Kiswahili · Kidato 2

Ufahamu…

Dakika 3 za kusoma ·

Yaliyomo

Ufahamu

  1. MAANA YA UFAHAMU

Ufahamu ni namna ya kulielewa jambo kwa ufasaha zaidi.

  1. DHIMA ZA UFAHAMU
  • Husaidia kuokoa muda.
  • Hupunguza gharama.
  • Huelimisha.

Mambo ya kuzingatia katika kazi ya ufahamu

  • Uzingatiaji wa habari kwa makini.
  • Kutambua mawazo makuu.
  • Kuonyesha welewa kwa njia ya usimulizi, maandishi au utekelezaji na kufuata maagizo.
  • Kuelewa vipengele anuai vya kifani kwa jambo linalounda kazi hiyo.
  1. AINA ZA UFAHAMU

Ufahamu wa kusikiliza

Huu ni aina ya ufahamu ambao husikiliza maelezo kutoka kwa mtu au watu wengine.

Mfano: Kusikiliza redio.

Mambo ya kuzingatia katika ufahamu wa kusikiliza

  • Kubaini mawazo makuu.
  • Kujua matamshi ya mzungumzaji.
  • Kusikiliza kwa makini.
  • Kuelewa lugha iliyotumika.

Ufahamu wa kusoma

Huu ni ufahamu unaotokana na maandishi ya kitabu, gazeti, jarida, vipeperushi pamoja na mabango.

Aina Za Usomaji

  1. Kusoma kwa sauti:

Hii ni namna ya kuyaangalia maneno na kuyatamka kwa sauti inayosikika.

Mfano: kusoma hotuba, risala, tangazo, au kumsomea mtu barua.

Mambo ya kuzingatia katika kusoma kwa sauti

  • Usahihi wa matamshi.
  • Mkazo (viimbo).
  • Alama za vituo.
  • Msito (gape fillers).
  1. Kusoma kimya:

Huu ni usomaji ambapo msomaji hupitisha macho katika maandishi bila kutoa sauti. Macho hayo huunganisha neno lililotangulia na linalofuata.

Faida za kusoma kimya

  • Hupima kasi ya msomaji na kiasi cha uelewa.
  • Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine.
  • Hukwepa kanuni za matamshi.
  • Huwezesha kusoma maneno mengi kwa muda mchache.
  1. KUSOMA KWA BURUDANI

Huu ni usomaji ambao lengo lake ni kujiburudisha tu.

Katika usomaji huu, msomaji husoma zaidi magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani.

  1. MBINU ZA KUJIBU MASWALI YA UFAHAMU

Ufahamu wa kusikiliza

  • Kuelewa matini.
  • Kuelewa swali.
  • Kujibu swali kutokana na matini.

Ufahamu wa kusoma

  • Kulielewa swali vizuri.
  • Kusoma habari yote kwa utulivu.
  • Kubaini jibu sahihi.
  • Kujibu swali kwa kutumia maelezo machache yaliyo muhimu tu, kwa kuzingatia kiini cha swali.
  1. UFUPISHO

Ufupisho ni maelezo yanayoandikwa kwa ufupi kutokana na habari fulani ndefu, bila kupoteza maana kamili ya habari hiyo.

Mbinu au taratibu za kufupisha habari

  • Kubaini mawazo makuu.
  • Kupanga maelezo kwa usahihi.
  • Kichwa cha habari.
  1. MATUMIZI YA KAMUSI

Kamusi ni mkusanyiko wa maneno katika kitabu, yaliyoandikwa kwa mpangilio wa alfabeti na kutolewa maana na maelezo mengine.

Kamusi hujumuisha mambo makuu mawili: vidahizo na vitomeo.

Vidahizo

Ni maneno yaliyoorodheshwa katika kamusi na kuandikwa kwa chapa iliyokoza.

Mfano: Aa.

Vitomeo

Ni neno au kidahizo pamoja na maelezo na taarifa zake zote anazohitaji mtumiaji wa kamusi.

Taarifa hizo ni kama zifuatazo

  • Aina ya maneno.
  • Wingi wa neno.
  • Fasili ya kidahizo.
  • Mfano wa matumizi.
  • Muktadha wa matumizi.
  • Matumizi katika misemo, nahau na methali.
  • Mnyumbuliko, hasa wa vitenzi.

Dhima au kazi ya fasihi katika jamii

  • Kuhifadhi msamiati.
  • Kuwa chanzo cha tahajia.
  • Kuwa chanzo cha sarufi ya lugha.
  • Kueleza matumizi sahihi ya maneno.
  • Hutumika katika utafiti wa historia ya lugha.

Mpangilio wa maneno katika kamusi

Maneno katika kamusi hupangwa kwa kufuata alfabeti.

Maneno yaliyo katika kategoria zaidi ya moja pia huingizwa katika kundi moja.

Mfano: Chuma1 na Chuma2.

Taratibu za utunzi wa kamusi ni kuteua misamiati.

Maswali

  1. Nini maana ya ufahamu?
  2. Kuna aina kuu ngapi za ufahamu? Zitaje.
  3. Taja mambo ya kuzingatia wakati wa kusikiliza habari au hadithi.
  4. Eleza maana ya ufupisho.
  5. Taja taratibu za kufupisha habari.
Jaribu quiz ya KiswahiliMaswali 39