Uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi
Dakika 2 za kusoma ·
Yaliyomo
Uhifadhi Wa Kazi Za Fasihi Simulizi
Umuhimu Wa Kazi Za Fasihi Simulizi
Kila utanzu wa fasihi simulizi una umuhimu wake katika jamii. Mfano ni kuelimisha na kuburudisha.
Pia fasihi ni nyenzo ya kutoa mafunzo kuhusu mambo kama vile
- dini
- historia
- siasa
- utawala
Vilevile, fasihi huwapa watu mazoezi na kuimarisha uwezo wao wa
- kuzungumza kwa ufasaha
- kuimba nyimbo kwa ufundi
- kuigiza mambo kwa ustadi
- kucheza ngoma kwa umahiri
Njia Za Kuhifadhi Kazi Za Fasihi Simulizi
Njia ya kichwani
Ubora wake
- Hufanyika wakati wowote bila maandalizi.
- Hauhitaji gharama za aina yoyote.
- Uwasilishwaji wake ni hai.
Udhaifu wake
- Huweza kupotea au kubadilika kwa urahisi.
Njia ya maandishi
Ubora wake
- Hudumu kwa kipindi kirefu.
- Huweza kuifikia hadhira iliyo mbali.
- Haipotezi fani yake na maudhui yake.
Udhaifu wake
- Hutumiwa na wanaojua kusoma na kuandika tu.
- Uwasilishwaji wake si hai.
Njia ya vinasa sauti
Ubora wake
- Huweza kuwafikia watu hata walio mbali.
- Haiwezi kupotea ikihifadhiwa vizuri.
Udhaifu wake
- Hutumia gharama.
- Uwasilishwaji wake si hai.
- Ni mali binafsi au ya msanii.
Njia ya kompyuta
Ubora wake
- Ni njia ya uhakika zaidi, na uwasilishwaji hufanyika pale panapohitajika.
Udhaifu wake
- Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya fanani na hadhira.
- Lazima msanii ajue namna ya kutumia kompyuta.
Njia ya kanda ya video
Ubora wake
- Huonesha wasanii.
- Hudumu kwa muda mrefu.
Udhaifu wake
- Kanda zisipotunzwa vizuri huharibika na kupoteza kazi za fasihi.
- Hakuna mawasiliano ya ana kwa ana baina ya fanani na hadhira.
Njia ya makazi
Njia hii hutumika kuhifadhi zaidi ala za kisanaa. Mfano ni ngoma, vinyago na mikeka.
Msanii huzikusanya kazi zake na kuzihifadhi nyumbani kwake. Hasa huzihifadhi katika nyumba zinazotumika kama maghala.
Ubora wake
- Kazi zinakuwa salama.
- Haihitaji gharama yoyote.
Udhaifu wake
- Ni rahisi kuharibika. Mfano ni mvua na moto.
- Ni rahisi kupotea kwa kuibiwa kama hakuna ulinzi.
Umuhimu Wa Kuhifadhi Kazi Za Fasihi Simulizi
- Ni sehemu ya ajira. Mfano ni maigizo na ngoma.
- Kuelimisha, kuburudisha na kuonya jamii.
- Ni vielelezo vya utamaduni.
- Hudumisha umoja na ushirikiano.
Maswali
- Eleza maana ya uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi.
- Uhifadhi wa kazi za fasihi kwa njia ya maandishi umeanza kutumika lini?
- Eleza ubora na udhaifu wa kuhifadhi kazi za kifasihi simulizi kwa njia ya maandishi.
- Pendekeza njia moja bora ya kuhifadhi kazi za fasihi simulizi na ueleze kwa nini.
Jaribu quiz ya KiswahiliMaswali 39
