Usimulizi
Dakika 1 za kusoma ·
Yaliyomo
Usimulizi
A: Maana Ya Usimulizi
Usimulizi ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu kuhusu tukio fulani.
B: Njia Za Usimulizi
Kuna aina kuu mbili za usimulizi. Ni hizi
- Usimulizi wa maandishi.
- Usimulizi wa mazungumzo au mdomo.
C: Taratibu Za Usimulizi Wa Matukio
Wakati wa kusimulia tukio, zingatia mambo yafuatayo
- Aina ya tukio. Mfano: tukio la harusi, wizi, ajali n.k.
- Mahali pa tukio. Mfano: kijijini, hospitalini, barabarani n.k.
- Wakati. Mfano: asubuhi, mchana, mwaka jana n.k.
- Wahusika wa tukio. Mfano: jinsia zao, umri wao n.k.
- Chanzo cha tukio.
- Athari za tukio, kama vile ajali. Mfano: je, watu wangapi wameumia?
- Hatima ya tukio. Mfano: hatima ya tukio la wizi ni mwizi kukamatwa na kupelekwa mahakamani.
Sehemu kuu za usimulizi wa tukio
- Utangulizi.
- Kiini.
- Mwisho.
D: Mbinu Za Usimulizi
- Uigizi, kama usimulizi ni wa mazungumzo. Mfano: uigizi wa sauti, matendo n.k.
- Usimulizi lazima uwe na kichwa cha habari. Kichwa hicho kiandikwe kwa herufi kubwa. Kisizidi maneno matano.
Maswali
- Nini maana ya usimulizi?
- Taja njia kuu mbili zinazotumika katika usimulizi.
- Taja sehemu kuu za usimulizi wa tukio.
- Usimulizi una mbinu zake. Zitaje.
- Eleza umuhimu wa usimulizi wa habari katika maisha yetu ya kila siku.
Jaribu quiz ya KiswahiliMaswali 39
