Kiswahili · Kidato 3

Uhakiki wa kazi za fasihi andishi

Dakika 47 za kusoma ·

Yaliyomo

Dhana ya uhakiki

  • Uhakiki ni uchambuzi au uchunguzi wa kina wa kazi ya fasihi kama vile riwaya, mashairi na tamthiliya kwa lengo la kufafanua kazi hiyo ili ieleweke vipengele vyake vya fani na maudhui.
  • Kuhakiki ni kama kufungua kifurushi kilichofungwa na kuanza kuchunguza vitu vilivyomo ndani yake, lakini pia chombo kilichotumika kufungia.
  • Kuhakiki, hujihusisha zaidi na kuichambua kazi ya fasihi katika vipengele vyote ya vipengele vya fani na maudhui, kuhakiki kazi ya fasihi hakuangali ndani ya fasihi tu bali huangalia hadi nje yake.
  • Muhakiki akishafanya uhakiki baadae huandika TAHAKIKI, kwa faida ya jamii kwa ujumla.
  • Uhakiki wowote wa kazi ya fasihi huzingatia maeneo makuu mawili maneno hayo ni fani na maudhui.
  • Kila eneo lina vipengele vyake ambavyo katika uchambuzi, huchambuliwa kimoja baada ya kingine.

Kuhakiki fani

Fani ni mbinu au ufundi anaotumia mwandishi wa kazi ya fasihi kufikisha ujumbe kwa hadhira au jamii ya watu iliyokusudiwa.

Vipengele vya fani ni pamoja na

  • Wahusika
  • Mandhari
  • Lugha
  • Muundo
  • Mtindo
  • Wahusika

Wahusika ni viumbe walio hai au wasio hai, halisi au wakufikirika wanatumika kufanya matendo mbalimbali katika kazi ya fasihi.

Kwa hiyo wahusika wanaweza wakawa Binadamu, Miungu, Mungu, Mawe,Mazimwi, n.k.

Kumbuka wahusika wote hutumika kuwakilisha tabia mbalimbali za binadamu kwani katika jamii zetu binadamu wote wanatabia tofauti tofauti, sasa kazi za fasihi zinatumia majina ambayo yanagusa baadhi ya tabia za hao watu.

Wahusika wanaweza wagawanyika katika makundi mawili ya wahusika wakuu na wahusika wadogo.

Mhusika mkuu ndiyo yule alieyebeba mawazo makuu ya mwandishi na pia huonekana kuanzia mwanzo hadi mwisho katika kazi ya fasihi.

Wahusika wadogo ni wale wanaonekana kwa uchache katika kazi ya fasihi.Mara nyingi wanatumika kumsahidia na kumdhihirisha mhusika mkuu.

Wahusika wakuu na wahusika wadogo katika kazi ya fasihi pia wamegawanyika katika makundi tofauti tofauti kama ifuatavyo:

  • 1.Wahusika mviringo (au duara)
  • 2.Wahusika bapa
  • 3.Wahusika shinda
  • Wahusika mviringo

Hawa ni wahusika ambao wanabadilika kitabia na kimawazo kulingana na hali halisi ya kimaisha.Kwa mfano wanaweza wakaanza na uovu wakamaliza na wema,pia wanaweza wakaanza na wema wakamaliza na uovu.

  • Wahusika bapa

Hawa ni wahusika ambao hawabadiliki kitabia kuanzia mwanzo hadi mwisho katika kazi ya fasihi.kwa mfano kama ameanza na uovu basi atamaliza na uovu wake na kama ameanza na wema basi atamaliza na wema wake.na kama ameanza na ulevi basi atamaliza kuwa mlevi.

  • Wahusika shinda

Hawa ni wahusika ambao wanayumbishwa kimawazo yani huwa kati ya wahusika bapa na wahusika mviringo.Wahusika hawa hawajitegemei kimawazo.

  • Mandhari

Mandhari ni sehemu au mahali ambapo matukio ya kazi ya fasihi yanatendeka.

Mandhari inaweza ikawa mandhari ya kijijini au mjini yani tunaangalia kazi ya fasihi imetendeka wapi.pia yaweza kazi ya fasihi imetendeka katika mandhari ya porini, hotelini au kwenye basi, vile vile kuna baadhi ya mandhari zakufikirika.

Hivyo basi tutachambua mandhari kwa kuangalia kazi ya fasihi imetendewa wapi (imefanyika wapi).

  • Lugha

Lugha ndio silaha kubwa msanii wa fasihi (mwandishi) kufikisha ujumbe wake kwa hadhira au jamii husika.

Kipengele muhimu sana katika matumizi ya lugha ni tamathali za semi,tamathali za semi zimegawanyika katika sehemu tofauti tofauti kama ifutavyo:

  • Tashbiha
  • Sitiari
  • Tashihisi
  • Mubalagha
  • Shtihizai
  • Tafsida
  1. Tashbiha

Huu ni ulinganishanishaji wa vitu au hali mbili kwa kutumia maneno kama vile,mithili ya ,mfano,sawa na nk.

  • 1.Anatembea mithili ya twiga
  • 2.Anajiamini kama mwanajeshi
  • 3.Pua yake ni sawa na sambusa
  1. Sitiari

Huu ni ulinganisho wa moja kwa moja wa vitu viwili bila kutumia maneno ya unganishaji kama vile,mithili ya ,kama,sawa.

  • 1.Wewe kweli mshamba.
  • 2.Elimu ni ufunguo wa maisha.
  • 3.Tiba bora kuliko kinga.
  • 4.Mchezaji yule ni kiboko kabisa.
  • 5.Joti na mpoki ni maswahiba wa karibu sana.
  1. Tashihisi

Ni hali ya kuvipa sifa vitu visivyo binadamu kuwa na sifa za kibinadamu,kama vile kusema,kulia,kucheka,nk.

  • 1.Miti ililalamika usiku kucha kwa upepo mkali.
  • 2.Mawe yaliunguruma kwa sauti kali kutoka juu ya milima.
  • 3.Hasira ya mawimbi iliwasambaratisha wavuvi wote.
  1. Mubalagha

Ni kueleza jambo kwa kutia chumvi.

  • 1.Mwana yule akikoroma mtaa mzima unasikia.
  • 2.Anatembea mithili ya twiga na sauti yake kama kinanda.
  • 3.Sikio la juma kama ungo wa kupetea mchele.
  1. Shtihizai

Ni maneno ambayo mtumiaji hutamka lakini humaanisha kinyume chake.pia huitwa kejeli

  • Kwa mfano mtaro wa maji taka unatoa harufu mbaya wewe ukasema mtaro huu unanukia.
  1. Tafsida

Ni maneno ambayo yanatumika kupunguza ukali wa maneno yani mara nying huwa ni maneno ya heshima na adabu.kwa mfano

  • 1.Amejifungua badala amezaa.
  • 2.Nikaingia uani badala ya nikaingia chooni.
  • 3.Kinyesi badala ya kusema mavi.

Pia zipo mbinu nyingine zilizo nje ya kundi la tamathali za semi.

Mbinu hizo ni pamoja na

  • Takriri
  • Tanakali sauti
  • Mdokezo
  • .Takriri

Ni kujirudia rudia kwa maneno.

Kwa mfano

  • 1.Nasema sitaki sitaki jambo ilo sitaki. Neno sitaki limejirudia.
  • 2.Nakupenda sana nakupenda sitokuacha nakupenda niamini.Neno nakupenda limejirudia.
  • Tanakali sauti

Ni kuiga kwa sauti ya kitu fulani.

Kwa mfano

  • 1.Akamwaga maji pwaaaaaaa!.
  • 2.Zilisikika karakacha! Karacha! za miguu yao walipofika kwenye majani makavu.
  • Mdokezo

Ni kuanzisha mazungumzo au wazo lakini unaishia njiani bila kulimalizia.

1.Juma: nitaku………………

2.Asha: utanifanyaje usini………………

Vilevile, fasihi hutumia ishara.Hizi ni taswira zinazojenga akilini, taswira hujenga kwa tamathali za semi.Mara nyingi matumizi ya taswira hujenga picha ya kitu fulani akilini mwa msomaji wa kazi ya fasihi .kwa mfano:

  • 1.Umauti ulitoa makucha yake meusi, ukakenua domo na kukaa tayaritayari kumrukia wakati wowote.

Japo umauti si jambo la kutisha ila maneno hayo yanatupa taswira ya jitu katili na la kutisha na lisilokuwa na huruma.

Mifano ya ishara

  • 2.Ngozi yake ikabadilika na kuwa sawa na ganda la ndizi.
  • 3.Sauti yake ilipenya masikioni mithili ya nyundo nzito masikioni mwa kila mtu.

Pia watunzi wa kazi za fasihi,pia hutumia semi katika kazi zao semi hizo ni pamoja na nahau,methali na misemo.

  • Nahau

Nahau ni usemi unaotumia maneno ya kawaida lakini lengo la kufikisha maana iliyo tofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo.kwa mfano ‘amevaa miwani’ ni nahau inayomaanisha amelewa

  • Methali

Ni semi fupi zinazobeba hekima ya jamii, ambazo aghalabu zimerithishwa kutoka vizazi vya nyuma.mifano ya methali ni kama vile ‘mwenda pole hajikwai’ na ‘mgagana upwa hali wali mkavu’

Methali hutumiwa kupamba lugha katika kazi ya fasihi.

  • Misemo

Misemo ni semi fupi fupi ambazo hutumiwa kwa kuleta maana maalum.

Kwa mfano: ‘amekuja juu kama moto wa kifuu’

  • Misimu

Haya ni maneno au semi zinazoibuka kwenye jamii,na hutumika na kutoweka kwa muda mfupi.

Kwa mfano: ‘kupiga pamba’,’vuta mkwanja’

  • Lugha nyingine

Kuna wakati mwandishi anaweza akatumia lugha tofauti tofauti katika kazi yake ya fasihi ili kuleta utamu wa kazi yake au kuleta utofauti wa kazi ama kuleta utofauti wa kielimu katika kazi yake ya fasihi.kwa mfano kuna baadhi ya kazi ya fasihi hutumia maneno ya lugha ya kigeni kama kiingereza.

  • Muundo

Muundo katika lugha ni mpangilio wa visa na matukio katika kazi ya fasihi.Hapa tunachunguza jinsi msanii wa kazi ya fasihi alivyounda na alivyounganisha tukio moja na jingine,kitendo kimoja na kingine,sura moja na nyingine.Tunapohakiki kazi ya fasihi kama riwaya,tamthiliya,kuna mambo ya kuzingatia.Mambo hayo ni:

  • Aina ya muundo
  • Mgawanyo wa kazi hiyo
  • Umbo la kazi hiyo

Aina Za Muundo

  • Kuna aina tatu za muundo.Aina hizo ni:
  • 1.Muundo msago.
  • 2.Muundo rukia.
  • 3.Muundo changamano.
  • 1.Muundo msago

Huu ni muundo wa moja kwa moja ambao visa na matukio vimepangwa katika hali ya kufuatana kuanzia tukio la kwanza hadi la mwisho.Pia huitwa usimulizi wa moja kwa moja.

  • 2.Muundo rukia

Ni aina ya visa na matukio.Hapa kuna kuwa na visa viwili au zaidi ambavyo hurukiana katika kusimuliwa kwake na mwisho wa visa hivi hugawana na kuwa kisa kimoja.Wakati mwingine muundo huu wa rukia huitwa muundo wa urejeshi, yani namna ya usimuliaji inayorukaruka hatua,yaani msimuliaji anaweza kuanzia katikati,akaja mwisho na kumalizia na mwanzo.Huu pia huitwa usimuliaji wa kioo.

  • 3.Muundo wa changamano

Huu ni muundo ambao kunakuwa na muundo wa msago na rukia.Hapa visa huanza kwa urejeshi/rukia na kumaliziwa na msago.Kwa mfano mwandishi anaweza kuanza sura ya kwanza hadi ya nne kwa msago,kisha akarejesha sura ya saba na ya nane kwa urejeshi/rukia,na ya sita akarudi kwenye msago.

Pia kipengele kingine cha muundo wa kazi ya fasihi ni ploti au msuko wa matukio,ploti ni mtiririko au mpangalio wa matukio wa kazi ya fasihi kwa namna inayofanya tukio moja lisababishe lingine na lingine n.k.

Ploti katika kazi ya fasihi hupitia hatua kadhaa.Kwa mfano,

  • Hadithi, huanza na utangulizi.Huu unaweza kueleza kuhusu mandhari au mhusika mkuu,
  • Kisha kufuata mgogoro.Hii ni hatua ambayo kunatokea kutokuelewana kati mhusika mmoja na mwingine,kundi na kundi au mhusika na nafasi yake.
  • Utata ni hatua ya tatu.Hapa,mgogoro unakuwa umepevuka na kuwa mkubwa.
  • Hatua ya mwisho ni hitimisho au suluhisho.Suluhisho ni hatua ambapo utata unapatiwa jawabu.

MGAWANYO WA KAZI HIYO.

  • Sura/namba = riwaya
  • Sehemu = tamthiliya
  • Idadi ya mstari kwa beti = ushauri

Ikumbukwe kwamba mwandishi anaweza kugawa kazi yake katika sehemu lakini akaipa picha sura na taswira.

Umbo La Kazi Hiyo

Katika kuangalia umbo la kazi ya fasihi mhakiki anapaswa kuelezea kama kazi hiyo ni riwaya, tamthiliya au ushauri.

  • Mtindo

Ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hutokeza au huonyesha nafsi na labda upekee wa mtunzi wa kazi hiyo. (Senkoro1982).

Wamitila (2003) naye anasema mtindo ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mwandishi kuwasilisha ujumbe wake.

Kwa ujumla, mtindo ni namna msanii au mwandishi anavyosimulia kazi hiyo.Hii ni namna kipengele cha lugha kinavyotumika.Kwa mfano matumizi ya nahau, methali na tamathali za semi.

Vile vile mtindo hubeba tabia binafsi za kiuandishi alizonazo msanii au mwandishi wa kazi husika ya fasihi na pia mtindo husaidia kumtofautisha msanii moja na mwingine au mwandishi mmoja na mwingine.

Jambo lingine linaloingia kwenye mtindo ni sauti, Sauti hizo mara nyingi huwa zinasimulia hadithi,husimuliaji huo huwa wa nafsi kwa mfano:

  • Nafsi ya kwanza.
  • Nafsi ya pili.
  • Nafsi ya tatu.
  • Nafsi ya kwanza.

Hii ni ile sauti inayosimulia hadithi ni ya mmoja wapo wa wahusika,yaani kwenye kikundi cha watu mmoja kati ya watu kwenye kikundi kile ndio anayesimulia hadithi.Kwa mfano:

‘Tulipompigia simu hakupokea kwa wakati ule, ila mwenzetu mmoja alimuona kwa mbali mtu yule’

  • Nafsi ya pili.

Katika usimuliaji huu mzungumzaji anamsemesha mtu mwingine ambaye wako naye.Nafsi hii hutumika zaidi katika dayalojia, hasa kwenye tamthiliya.Kwa mfano:

‘Saidi mbona uliniambia kuwa utanilipa leo deni langu’

  • Nafsi ya tatu.

Huu ni usimuliaji ambao,msemaji si mmoja wa wahusika,bali ni mtazamaji anayetoa ripoti kuhusu yale anayoyaona au anayoyajua. Kwa mfano

‘Polisi walipofika pale hawakukuta mtuhumiwa wanaemuhitaji lakini wakamchukua mke wake’

Kuhakika maudhui

Maudhui ni mambo yote anayosema msanii au mwandishi wa kazi ya fasihi kwa walengwa wake au hadhira yake ama jamii iliyomzunguka.Katika kuhakiki maudhui, vipengele vya kuzingatia ni:

  • ,.Dhamira

Hili ni wazo kuu katika kazi ya fasihi na siku zote dhamira kuu ndilo wazo alilonalo mwaandishi au msanii wa kazi wa fasihi.Msanii huwa na dhamira fulani ambapo anataka kuiwasilisha kwa jamii au hadhira iliyomzunguka hivyo hutumia kazi ya fasihi kufikisha dhamira yake.kwa mfano mwandishi anaweza kuhusu ukombozi wa mwanamke,rushwa,umuhumi wa elimu ata mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu.

Pia kuna dhamira ndogo ndogo ambazo zinajitokeza hapa na pale ndani ya kazi ya fasihi na mara nyingi hujitokeza kila sehemu kwenye kazi ya fasihi,mara nyingi huwa ndizo zinatumiwa kujibu maswali ya dhamira ndogo ndogo ambazo hujitokeza katika jamii zetu.Kwa mfano mwandishi anaweza akazungumizia masuala ya ulevi,ndoa za utotoni,rushwa,ndoa za wake wengi,unyanyasaji,utapeli,magonjwa mbali mbali kama ukimwi,unasikini,manyanyaso,n.k.

  • Ujumbe

Hizi ni taarifa ambazo msanii au mwandishi wa kazi ya fasihi huzitoa kwa jamii au hadhira yake.Taarifa hizo mara nyingi hubeba mafundisho kwa jamii husika yaani baada ya kusoma kazi ya fasihi unapata fundisho gani, fundisho hilo ndilo tunaita ujumbe.Kwa mfano ‘siku za mwizi arobaini’ ina ujumbe kwamba lenye mwanzo lina mwisho wake.Ikumbukwe kwamba kazi moja ya fasihi inaweza ikawa na ujumbe zaidi ya mmoja.

  • Falsafa

Falsafa ni mawazo makuu ya msanii (mtunzi) wa kazi ya fasihi kuhusu maisha ya binadamu kwa ujumla.Mawazo haya hutokana na uchanganuzi wa kimantiki na huwa ndiyo hekima na busara ya msanii au mtunzi wa kazi ya fasihi.

Pia falsafa ni msimamo wa mwandishi au msanii katika maisha juu ya utatuzi wa matatizo katika jamii.Unaweza kuijua falsafa ya mwandishi kwa kusoma kazi zake tofauti tofauti,yaani kazi zaidi ya moja.

  • Mtazamo

Mtazamo ni kigezo ambacho mwandishi anakitumia katika kuyatazama mambo mbali mbali ya maisha.Kwa Mfano; mtazamo wa kidini unaweza kumwongoza kuona kuwa,kila jambo ni mapenzi ya Mungu.Mtazamo wa kisayansi,kwa upande mwingine,utayaona maisha kuwa ni matokeo ua juhudi binafsi za mwanadamu.

  • Migogoro

Hi ni mivutano au kutoelewana ama kukubaliana kuhusu mambo mbalimbali kati ya muhusika mmoja na mwingine,muhusika na kikundi cha watu fulani,kundi la watu fulani na kundi lingine,kikundi cha watu fulani na jamii,muhusika na jamii, muhusika na nafsi yake (tunaita mgogoro wa nafsi).Pia kuna aina mbali mbali za migogoro.Aina hizo ni pamoja:

  • 1.Migogoro ya kisiasa

Hii ni migororo inayotokana na tofauti za kisiasa miongoni mwa wahusika wa kazi ya fasihi.

  • 2.Migogoro kiuchumi

Hii inatokana na mivutano ya kugombania rasilimali au kutokana na ukandamizaji na unyonyaji unaotendwa na tabaka la juu au wale walio nacho dhidi ya wasio nacho au tabaka la chini.

  • 3.Migogoro ya kijamii

Hii ni migogoro inayotokana na kupishana katika uzingatiaji wa mila, desturi na taratibu zinazokubalika katika jamii fulani.

  • 4.Migogoro ya kinafsia

Hii ni migogoro inayotokea kati ya mhusika na nafsi yake mwenyewe.Hali hii huweza kutokea pale ambapo anakuwa njia panda kwa kushindwa kuamua kati ya pande mbili au mawazo mawili yanayomkabili, huku akitakiwa kufanya uamuzi.

  • Msimamo

Neno ‘msimamo’ maana yake ni maoni aliyonayo mtu juu ya jambo fulani.Msimamo wa mwaandishi ni maoni yake juu ya mambo mbalimbali anayoyaeleza kwenye kazi yake.Mathalani,kama kazi ya fasihi inagusia mfumo wa siasa katika nchi,msimamo wa mwandishi unaweza kuwa ni kuunga mkono mfumo wa vyama vingi au wa chama kimoja.

  • Mafunzo

Mafunzo ni mambo tunayojifunza kutokana na kusoma kazi ya fasihi.Hapa tunaangalia baada ya kusoma kazi ya fasihi tunapata funzo gani.Mfano mhusika anaweza akapata tabu sana katika maisha yake, ata kufikia hatua ya kudharauliwa lakini baadae akafanikiwa na kusahau tabu zote, hivyo basi funzo tunalolipata hapa ni kwamba mvumilivu hula mbivu.

Kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi.

Kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi kunategemea zaidi jinsi mwandishi alivyoweka uwiano wake mzuri kati ya fani na maudhui kwa namna ambayo inaleta uhalisia.Kwa mfano msanii anaweza akamtumia mtoto wa miaka mitano na kutumia misemo mizito tofauti na umri wake hapo tunasema msanii hajafaulu.

Kuhahiki riwaya.

Riwaya ni hadithi ndefu yenye mtirirko wa visa, mandhari mapana na wahusika wengi na iliyosimuliwa kinathari.Yapo mambo ya kuzingatia pindi unapohakiki riwaya na mambo hayo yamegawanyika katika vipengele vya fani na maudhui.Yafuatayo ni mambo muhimu katika uhakiki wa riwaya:

Fani

  • 1.Wahusika

Katika kuchambua wahusika yakupaswa muhakiki kuangalia undani wa wahusika na kujiuliza maswali kadha wa kadha kama ifuatavyo;

  • a.Wahusika hao ni wakuu au wadogo?
  • b.Wao wanasemaje?
  • c.Wahusika wengine wanasema nini kuwahusu?
  • d.Mwandishi anawaelezeaje?
  • e.Wanatenda matendo gani?
  • 2.Mandhari

Kuna mambo ya kujiuliza kwenye kuhakiki mandhari kama yafuatayo

  • a.Je mandhari ni ya wapi ya kijijini au mjini?
  • b.Je maneno yanayoongelewa na wahusika yanaendana na mandhari husika.
  • 3.Lugha

Katika uchambuzi wa lugha muhakiki ajiulize maswali yafuatayo

  • a.Je mwandishi ametumia lugha za kigeni?.
  • b.Je kuna matumizi ya lugha za ishara ?
  • c.Je mwandish ametumia tamathali za semi?
  • d.Je mwandishi ametumia lugha inayoeleweka au lugha ngumu ?
  • 4.Muundo

Mhakiki anapaswa kujiuliza maswali yafuatayo

  • a.Je, riwaya imegawanyika katika sura ngapi?
  • b.Je usimulizi wake ni wa moja kwa moja au wa urejeshi?
  • c.Je mwandishi katika riwaya iyo ametumia ushairi au dayalojia ndani ya hadithi?

Maudhui.

  • 1.Dhamira

Maswali ya kujiuliza ni haya yafuatayo

  • a.Ipi ni dhamira kuu ya riwaya hiyo?
  • b.Dhamira ndogo ndogo ni zipi?
  • 2.Ujumbe

Mambo ya kijiuliza katika kuhakiki ujumbe kwenye riwaya

  • a.Tunapata funzo gani kutokana na dhamira kuu?
  • b.Tunapata funzo gani kutokana na dhamira ndogo ndogo?
  • 3.Falsafa

Katika kuhakiki falsafa kwenye riwaya mambo yafuatayo ni muhumu kujiuliza;

  • a.Mwandishi anaamini nini kuhusu maisha kwa ujumla?
  • b.Je, falsafa hiyo ina ukweli au la? Kwa nini?
  • 4.Mtazamo

Ili kuhakiki mtazamo wa mwandishi wa riwaya, tunajiuliza maswali yafuatayo

  • a.Je,mwandishi ana mtazamo wa kisayansi (Kiyakinifu)
  • b.Je, mwandishi ana mtazamo wa kidhanifu yaani wa kidini, utakuta mwandishi anaamini kwenye Mungu au Miungu.
  • 5.Migogoro

Tunapohakiki kipengele cha migogoro katika riwaya, tunajiuliza maswali yafuatayo

  • a.Kuna mgogoro kati ya mhusika mmoja na mwingine?
  • b.Kuna migogoro kati ya mhusika mmoja na kundi,kwa mfano jamii?

Uhakiki wa Fani katika riwaya ya Takadini

Mwandishi: Ben J. Hanson

Wachapishaji: Mathews Bookstore And Stationaries

Mwaka: 2004

Jina La Kitabu

Jina la kitabu TAKADINI lina maana ya “Sisi tumefanya nini”. Hili ni jina ambalo Sekai alimpa mwanae mara baada ya kumzaa. Jina hili lilitokana na majonzi aliyokuwa nayo juu ya kutaka kuuawa kwa mwanae na yeye ilihali hawakuwa na hatia, ila tu kwa sababu ya mila za jamii yake zilivyotaka. Jina hili la kitabu ni sadifu kwani linasawiri vyema maudhui yaliyomo katika kitabu hiki. “Sisi tumefanya nini?’ ni swali ambalo linatokana na ukosefu wa haki ya kuishi, kubaguliwa kutopendwa, na hata kutengwa kwa watu wenye matatizo katika jamii. Swali hili linawalelekea wanajamii ambao bado wanashikilia mila potofu zinazowakandamiza na kuwanyanyasa watu wenye matatizo mfano, ulemavu wa ngozi, wagonjwa nk. Jina hili pia ni sadifu kwa maisha ya jamii yetu ya watanzania kwani watu bado wanashikilia mila potofu ambazo si nzuri. Mwandishi ametumia jina hili makusudi ili kutaka kuionesha jamii hali halisi ya vilio vya albino, wasichana wadogo wanaolazimishwa kuolewa nk. Kuwa huu sasa ni muda mwafaka wa jamii kuyaacha na kutupilia mbali mambo hayo.

Muundo

Muundo alioutumia mwandishi wa riwaya hii ni muundo wa msago au kwa jina lingine muundo wa moja kwa moja. Ameyapanga matukio katika mtiririko sahili kwani ameanza kutuonesha toka mwanzo mpaka mwisho wa maisha ya kijana Takadini “Msope”.Toka kutungwa kwa mimba yake, kuzaliwa kwake na kuishi kwake, matatizo na changamoto zinazomkumba na jinsi anavyokabiliana nazo na hatma ya maisha yake.

Mgawanyo wa visa na mtukio umepangwa katika sura ambapo visa vimejengwa kwa ufundi na kuvifanya vijengane na kukamilishana kuelekea kilele cha masimulizi. Matukio haya yamewekwa katika sura kumi na tatu.

  • Sura ya Kwanza:Sura hii inaanza kutuelezea kuhusu mwanamke Sekai anavotunga mimba, pia tunaelezwa kuhusu mtazamo mbaya wa wake wenzie juu ya mimba hiyo baada ya Sekai kukaa kwa muda mrefu bila ya kujaliwa mtoto.
  • Sura ya Pili:Hapa tunasimuliwa jinsi Sekai anavyofanikiwa kujifungua salama. Lakini kwa bahati mbaya kwa kawaida ya jamii yao anajifungua mtoto Zeruzeru ambaye kwa mila zao mtoto huyo ni laana. Hivyo alipaswa kutupwa mara moja ama kuuawa. Hakuna ambaye alikuwa tayari kumpokea mtoto yule kwani si baba yake wala jamii yake ila mama yake pekee.
  • Sura ya Tatu:Jamii bado haipo tayari kumpokea mtoto Sope, wanawake wenza wa Sekai wanasubiri kwa hamu kuona tukio la kutupwa kwa Takadini litakavokuwa, kwani ndio jinsi mila na taratibu za mababu zilivyotaka. Kutokana na hali hii ndipo Sekai anapata wazo la kutoroka. Anaamua kuondoka kwenda mbali ili kukinusuru kichanga kisicho na hatia kwani alisubiri kwa hamu na uchu wa muda mrefu kupata mtoto.
  • Sura ya Nne:Sekai anafanikiwa kutoroka na mwanae Takadini ili kumuepusha na kifo, jamii na Mtemi wanapata habari ya kutoroka kwake. Upelelezi unafanyika lakini juhudi hazikuzaa matunda kumpata Sekai na mwanae mchanga waliotakiwa kuuawa. Sekai anasafiri mbali na kufikia kijiji kingine na kupokelewa na mzee Chivero.
  • Sura ya Tano:Sekai anapokelewa katika kijiji cha mzee Chivero, jamii na wazee wanashitushwa sana na ujio huo lakini wanalazimika kumpokea tu baada ya malumbano ya muda mrefu. Kwani mila ziliwataka kutowatelekeza wageni katika kijiji chao, na hiyo ndiyo inakuwa mwanzo wa matumaini ya Sekai kuhusu kuishi kwa mwanae ambaye alionekana kuwa ni laana ya mababu na hakupaswa kuishi.
  • Sura ya sita:Baada ya Sekai kupokelewa katika kijiji cha mtemi Masasa, habari za ujio wake zinaenea kwa wanakijiji wote na wanaonekana kushtushwa sana, si hivo tu bali pia wanajiapiza katu kutomsogelea Sope kwani waliamini amelaaniwa. Lakini kwa juhudi za mzee Chivero baba mpya mlezi wa Takadini Sekai anapata rafiki. Tendai mke wa mtemi Masasa. Anajengewa kibanda cha kuishi yeye na mwanae na maisha yanaanza.
  • Sura ya saba:Sekai anaanza kujishughulisha na shughuli za kawaida kama mama na mwanamke, analima bustani na kufanya kazi ndogo za nyumbani. Siku moja katika safari ya kurudi nyumbani kwa bahati mbaya wanavamiwa na nyuki na kujeruhiwa vibaya yeye na mwanae, anaamua kumtupia mwanae kichakani ili kumuokoa na yeye kujitumbukiza mtoni. Wote wawili wanafanikiwa kutibiwa na kupona majeraha.
  • Sura ya nane:Taratibu Takadini anaanza kukua lakini anagundulika kuwa hawezi kutembea vyema kwa mguu mmoja, hii ilitokana na kuvunjika Mguu baada ya kurushwa kichakani na mamaye kama juhudi za kumwokoa. Hali hii inamhuzunisha zaidi Sekai na Chivero kwani walimpenda sana. Hapa ndipo mapenzi ya Chivero yalianza kudhihirika rasmi kwa Takadini kwani alijenga urafiki naye na kumpenda kama mwanae. Alimfundisha utabibu wa dawa za kienyeji na mambo mengine mengi. Pia tunaona watoto jinsi walivyombagua Takadini kutokana na hali yake, kwani waliambiwa na wazazi wao wasicheze naye amelaaniwa hivo hawakuthubutu.
  • Sura ya tisa:Katika sura hii, Mzee Masasi anafariki dunia na kumuacha mzee Chivero katika majonzi makuu. Hali ya mzee Chivero nayo inaanza kuzorota kwa uzee. Anampa Takadini usia mbalimbali na kumfunza. Pia tunaelezwa juu ya fikra mpya za Takadini za kupiga “mbira” kifaa cha muziki cha kijadi, hii baada ya kuvutiwa na sanaa hiyo aliposhiriki sherehe za mavuno za mwaka. Jamii bado ilimtenga Takadini na kumbagua, walimwona si binadamu bali mzuka tu! Na kwa bahati mbaya mzee Chivero naye aliaga dunia na kuacha simanzi kuu kwa Sekai na Takadini mbao alikuwa ni tegemeo na faraja kwao.
  • Sura ya kumi:Baada ya kifo cha mzee Chivero, Takadini anapata mwalimu maarufu mpiga mbira mzee Kutukwa, anamfundisha kupiga mbira, Takadini anaonesha juhudi kuu na kufanikiwa. Pia anmsaidia kifaa cha kumsaidia kutembea kutokana na mguu wake mbovu, hii inakuwa ni faraja kubwa kwa Takadini na mamaye.
  • Sura ya kumi na moja:Hapa tunaelezwa juu ya kijana Nhamo adui mkuu wa Takadini kwani hakumpenda na alimdhihaki na kumdhalilisha mara kwa mara. Kijana huyu anaonekana kuwa ni shujaa katika jamii yake kwa kitendo cha kumuua simba mla mifugo. Hiyo inamletea sifa kubwa na majivuno mengi hivo wasichana wengi kumtamani awaoe, hali ni tofauti kwa Shingai ambaye anaonesha hisia za mapenzi kwa Takadini pamoja na hali yake ya “Usope”. Chemchemi za mapenzi ya Takadini kwa Sekai zinaanza kumea jambo ambalo linamkera sana Nhamo na kuzidisha chuki kwa Takadini kwani pia alitamani kuwa na Shengai binti mrembo. Jamii inafanya kikao kujadili suala la Shengai kumpenda Takadini na wanalipinga vikali suala hilo.
  • Sura ya kumi na mbili:Nhamo anakata shauri na kwenda kumposa Shengai, wazazi wa pande zote mbili wanaliunga suala hilo mkono asilimia zote. Kwani hilo lingewanusuru aibu ya mwanao kuolewa na Sope, kwani walijua fika Shingai alimpenda Takadini na hakumtaka Nhoma. Nhoma anamuonya vikali Takadini kuwa asiendelee na lolote kwa Shengai. Pia hapa zinafanyika sherehe ya kijadi ya kumkaribisha hayati mzee Chivero tena nyumbani.
  • Sura ya kumi na Tatu:Wakati wa sherehe ya mavuno, binti Shengai anashindwa kuvumilia na kuamua kumfuata Takadini kibandani kwake. Anaamua kuvunja mila za kwao kwani alimpenda kwa dhati Takadini, pamoja na dharau, kejeli, kubaguliwa, ulemavu wake na kuonekana kuwa ni mtu aliyelaaniwa. Wazazi wake wanamtenga na kutomtambua kama ni mtoto wao tena. Suala hilo linatikisa jamii ya watu wa kijiji kile na hata kutaka kuwafukuza Sekai na mwanae lakini wanaokolewa na maamuzi ya busara ya wazee kwa kuwacha Shengai na mpenziwe Takadini waishi hali wakisubiri matokeo! Kuwa je mtoto atazaliwa sope? Na kuongeza ukoo wa masope na kijiji chao kuwa cha masope? Hapa ndio inapojulikana hatma ya Takadini na mkewe kwani anapata ujauzito na kufanikiwa kujifungua mtoto salama asiye Sope. Ilikuwa furaha kuu kwa mama na mtoto na wote pia. Wanaamua kurudi kijijini kwao walikotoroka ili kwenda kuwadhihirishia kuwa hata sope anaweza kuishi hapaswi kubaguliwa na kutengwa

Mtindo

Mwandishi ametumia mitindo kadha wa kadha ili kuipamba kazi yake na kuifanya ivutie wasomaji; mfano matumizi ya nafsi mbalimbali, matumizi ya nyimbo nk.

Matumizi ya nafsi

Kwa kiasi kikubwa yametawala matumizi ya nafsi ya tatu umoja na wingi katika sura zote.Mfano.uk. 30. “ aliingia ndani na kuanza kazi.”Piauk.3 “ Sekai alikoka moto nje ya kibanda, akaketi na kuzungumza na Pindai”.

Matumizi ya nafsi ya pili au dayalojia

Mfano uk 29 - 30. Mazungumzo kati ya Chivero na Sekai:“je umelala salama?“je umelala salama?Sijambo mwanangu, sijui wewe?Sijambo Sekuru,Na mwanao je?Naye hajambo.”

Matumizi ya nafsi ya kwanza. Mfano uk. 82 na 83

“lakini ghafla nilipata nguvu mpya”;“nilikuwa na nguvu kama kijana….”

Pia mwandishi ametumia nyimbo katika baadhi ya sura ili kuwaburudisha na kuliwaza wasomaji. Mfano uk. 2 wimbo aliouimba mke mwenza wa Sekai Rumbdzai.

“Mashamba yetu yamelimwa mbegu nazo zimepandwa zimechipua na kumea, sisi watatu tumepanda mavuno yetu; mheshimiwa wetu amemiliki mavuno kwa mikono yake halisi kutoka mashamba yetu yote lakini ni kipi alichoambulia kutoka ardhi ile isiyomea kitu?”pia ametumia wimbo uk. 34, 57, 85.

Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi pia ni mtindo mwingine wa usimulizi alioutumia mwandishi.Mfanouk82Kutukwa alisimulia vijana hadithi enzi ya ujana wake na jinsi alivopambana na maadui vitani.

Matumizi ya Lugha

Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na rahisi inayoeleweka kwa wasomaji wake. Ametumia pia lugha nyinginezo kama vile lugha za kikabila.Maneno kama vile“Amai”,lenye maana yamama, “Sope”lenye maana yazeruzeru, “shumba”- simba, “mbira” – chombo cha asili cha muziki, “gudza” – blanketi lililotengenezwa kwa nyuzi za magome ya miti.nk.Hivyo mwandishi ametumia lugha hii ili kuwaleta wasomaji kwenye mazingira halisi ya kiutamaduni ya jamii ile.

Matumizi ya tamathali za Semi

  • Tashibiha:Mfanouk. 6 “ muda huenda polepole mithili ya mwendo wa kakakuona Uk.15 “ habari njema huchechemea kwa mguu mmoja lakina mbaya hukimbia kama Sungura”Uk.16 “….. alibaki kama kinyago cha mpingo”.Uk.28 “ sio kufurika kama Chura”Uk.33 “aligeuza shingo yake sawa na Mbuni”Uk.42 “ nywele kama vinyweleo vya mahindi yaliyokaribia kukomaa”Uk.82 “muziki ulikuwa kama chemchemi ya maji mwilini mwake”
  • Tashihisi:Mfano uk. 5 “ndege mbalimbali wakiimba kuikaribisha siku mpya”Uk. 7 “vivuli vya jioni viliongezeka urefu”Uk. 18 “maneno yananila mifupa yangu”Uk 25 “kifo kilinukia”
  • Tafsida:Mfano, uk. 83 “sehemu zake za siri”
  • Sitiari:Mfano, uk. 88 “Tapfumaneyialigeukambogo” Uk.97“mwana Mbwa hakuiba mfupa”, Tawanda mfupa ulikwenda wenyewe kuchezanaye.” Hapa mfupa umefananishwa na Shingai na Takadini ndio mwanambwa

Matumizi ya Semi

  • Methali:Uk. 45 “ kipofu huwa hachagui shimo la kutegea wanyama”uk.33 “ moyo mwema utakufanya uuwawe”Uk 79 “Baba , motto asiyelia hufa na njaa”
  • Misemo:Mfano.Uk. 12 “kufikiri katika siri ni sawa na safari ya mbwa”Uk. 100 “kanga hawezi kutua juu ya bua la mtama”Uk.101 “kibuyu kikubwa hakikosi mbegu ndani”Uk. 125 “fuvu la nyanilimekuwa kijiko kwa mlo wa mahindi”
  • Nahau:uk. 27 “ penzi langu kwake halikufua dafu”Uk. 88 “kutiana moyo wa ari”

Matumizi ya mbinu nyinginezo za kisanaa

  • Nidaa:Mfano,Uk.4 “Ha!” , “Ha! Atimuliwe tena? Mchawi?” Uk.16 “Mai, Wee!” Uk.39. “Ha! Iwe! Ha!”
  • Mdokezo:MfanoUk.3 “ndiyo Pindai, ninaogopa……….” Uk.42 “mtu mzima kama watu wenine ameamua………”
  • Takriri:Mfano,uk 57 “ mwanangu, mwanangu, mwanangu, wamekufanya nini?”

Wahusika

Sekai

  • Ni mke wa Makwati wa kwanza.
  • Ni mwanamke jasiri.
  • Anapinga mila potofu na mbaya za jamii yake.
  • Ni mvumilivu.
  • Ni mchapakazi mzuri.
  • Anajifungua mtoto zeruzeru ambaye ni laana kwa jamii yake.
  • Ni mtiifu na mwenye adabu.
  • Ana huruma na mnyenyekevu.
  • Ana mapenzi ya dhati.
  • Anafaaa kuigwa na jamii.

Takadini

  • Ni mtoto anayezaliwa na ulemavu wa ngozi( albino)
  • Anasadikika kuwa ni laana kwa jamii yake hivyo kupaswa kuuawa au kutupwa mbali.
  • Anaokolewa na mama yake kwa kutoroshewa katika kijiji kingine.
  • Anapokua anakua kijana jasiri.
  • Hapendwi na jamii.
  • Anabaguliwa na jamii, hana rafiki.
  • Ni mvumilivu na msikivu mwenye heshima.
  • Alimpenda Chivero sana.
  • Alikuwa mpiga mbira (chombo cha muziki cha kijadi) maarufu.
  • Alimuoa Shingai na kupata mtoto asiye Sope.

Makwati

  • Mume wa Sekai.
  • Ameoa ndoa ya mitara ana wake wanne.
  • Anashikilia mila na desturi potofu.
  • Hana mapenzi ya dhati kwa mwanae.
  • Hafai kuigwa na jamii.

Dadirai na Rumbidzai

  • Wake wengine wa mzee Makwati.
  • Wana wivu.
  • Hawampendi Sekai.
  • Wana roho mbaya kwani wanamwombea Sekai mabaya.
  • Ni katili kwani wanashinikiza Sekai na mwanae wauawe bila huruma.
  • Wasengenyaji.
  • Hawafai kuigwa na jamiii.

Pindai

  • Mke wa pili wa Makwati.
  • Ana upendo wa dhati kwa Sekai.
  • Ni mkweli.
  • Hana wivu.
  • Ni mshauri mzuri.
  • Anafaa kuigwa na jamii.

Chivero

  • Ni mzee wa kijiji cha mzee Masasa.
  • Anawapokea Sekai na mwanae baada ya kutoroka kwao kwa ukarimu mkubwa.
  • Ni mwenye roho nzuri.
  • Ana huruma sana.
  • Ni mganga wa tiba za asili.
  • Ana mapenzi ya dhati kwa Takadini na Sekai.
  • Anamrithisha Takadini uganga.
  • Ana busara na hekima.
  • Ni mshauri mkuu wa Mtemi Masasa.
  • Anafaa kuigwa na jamii.

Mtemi Masasa

  • Ana busara na hekima.
  • Ana huruma.
  • Anafuata mila na desturi ya jamii yake.
  • Ni msikivu.
  • Ni rafiki mkubwa wa Chivero.
  • Ni kiongozi bora.

Nhamo

  • Ni kijana katika kijiji cha mtemi Masasa.
  • Ana majivuno na jeuri.
  • Hampendi Takadini kwani alimbagua kumpiga na hata kumdhalilisha.
  • Hafai kuigwa n ajamii.

Tendai

  • Mke mdogo wa mwisho wa mtemi Masasa.
  • Aliolewa bila kupenda, hakumpenda mtemi Masasa kwani alimzidi umri.
  • Alikuwa rafiki mzuri wa Sekai.
  • Ana mapenzi ya dhati kwa Takadini.
  • Ana bidii na mvumilivu.

Nhariswa na mkewe

  • Ni wazazi wa Shingai
  • Wanashikilia mila desturi potofu
  • Hawakupenda kabisa kitendo cha mtoto wao kumpenda Takadini
  • Walimlazimisha kuolewa na Nhamo kwani walitaka sifa na maujiko
  • Walimtenga Shingai baada ya kutoroka na kuolewa na Takadini
  • Si wazazi wazuri
  • Hawafai kuigwa na jamii

Kutukwa

  • Ni mzee katika kijiji cha mtemi Masasa
  • Ni mpigaji mbira maarufu
  • Alimfundisha Takadini kupiga mbira
  • Alitoa mtazamo mbaya kwa wanakijiji wenzake kwa kuwaeleza sifa nzuri za Takadini
  • Alimpenda Takadini. Anafaa kuigwa na jamii

Mandhari

Mandhari aliyotumia Ben J Hanson ni mandhari ya kijijini kwani maisha ya watu na mazingira yanayoelezwa ni ya kijijini, masuala kama ya kilimo, ufugaji, sherehe za mavuno, makazi ya watu kukaa katika jumuiya ya pamoja kijamaa inayoongozwa na mtemi mmoja. Mfano mtemi Masasa, yote haya ni viashiria kuwa mandhari ni ya kijini. Mandahari ambayo mwandishi ameijengea mawazo yake na kuyaibua ni sadifu na halisi. Kwani maeneo ya vijijini ndiko kulikokithiri mambo ya imani potofu na za kishirikina kama vile kuwaua watoto Sope au albino.

Maudhui

  • Dhamira
  • Mabadiliko ya kifikira

Mabadiliko ya kifikira katika riwaya hii ya Takadini ndio dhamira kuu.mwandishi anajaribu kuonyesha baadhi ya tamaduni ambazo zmierithishwa kizazi hadi kizazi lakini zinzhitajika kuachwa au kubomolewa sababu hazina faida yeyote katika jamii zetu.miongoni mwa fikira hizo zimepitwa na wakati kwan kuna baadhi ya jamii zinaamin kwamba kuwa na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ni mkosi ambacho kitu si cha kweli na hakina mashiko.Katika kitabu cha Takadini tunaona jamii ilikua inaamini kuwa mtoto akizaliwa albino inabidi auwawe yaani kwao wao albino au mlemavu wa ngozi ni mikosi,ilifikia hatua mpaka Takadini kutengwa na jamii yake.

Baada ya kuangalia dhamira kuu sasa ni wakati wa kuangalia dhamira ndogo ngogozilizojitokeza kwenye riwaya ya Takadini, kama ifuatavyo:

  • Suala la Unyanyapaa

Mwandishi wa kazi hii ya fasihi anajaribu kuonesha jinsi gani watu wenye matatizo fulani wanavyonyanyapaliwa na jamii zao kwa mfano katika (Ukurasa wa 22) Makwati ana mnyanyapa Sekai sababu ya ugumba yaani sababu hazai.

Pia dhamira hii ya unyanyapaaji imejitokeza katika riwaya pale jamii inapomtenga Takadini kwa sababu ya ulemavu wa ngozi ya albino au sope,tunaona watoto wenzake Takadini wanamnyanyapaa pale anapojaribu kucheza nao na ata anapojaribu kuwaimbia nyimbo.pia aya matatizo ya kunyanyapaa na kuwauwa watu wenye ulemavu wa ngozi huwa yanatokea kwa wingi sana na miongoni mwao kuwaamini kwa watu wenye ulemavu wa mwili wanawaletea utajiri na kuanza kuwauwa au kuwakata viongo vyao na kuna jamii nyingine zinawauwa kabisa watu wenye ulemavu wa ngozi.

  • Suala la Mapenzi

Mwandishi anaonyesha mapenzi ya kweli na mapenzi yasiyo ya kweli yaani ya kulazimishana,tunaona jinsi gani shingai alivyokuwa na mapenzi ya kweli nay a dhati kwa kijana Takadini hadi kufikia hatua ya kudharaulika na jamii nzima ya kijijini kwao lakini alikubali kuolewa na Takadini ambaye ni mlemavu wa ngozi na kuwakataa wengine ambao si walemavu wa ngozi.mapenzi ya dhati pia hutokea kwenye jamii zetu tunazoishi wapo wanawake wanakubali kuolewa na wanaume mafukara,maskini,walemavu na kufanya nao maisha.

Lakini kwa upande mwngine tunamuona Tendai, mke mdogo wa mtemi masasa akiwa hana furaha ya kuolewa kwa ndoa kwani ndoa yao haikutokana na mapenzi ya kweli.pia kwenye jamii zetu za kawaida hizi tunazoishi mambo kama haya huwa yanatokea kwani kuna baadhi ya wazazi huwa wanatabia ya kulazimisha watoto wao kuolewa na watu wenye uwezo lakini kati yao kuna hakuna mapenzi ya dhati.

  • Nafasi ya mwanamke katika jamii

Pia mwandishi amejaribu kuonyesha nafasi ya mwanamke katika jamii yani amemuonyesha mwanamke kama mtu ambae ndio chachu ya maendeleo katika jamii na mwanamke kama mtu jasiri.

Mwanamke mwingine jasiri ni Shingai pale alipokubali kuolewa na Takadini na kubadili fikra za wanajamii kwamba albino ni mtu kama watu wengine.

  • Suala la imani potofu

Jamii ya kina Sekai inaamini kuzaa mtoto albino ni mkosi hii ni imani potofu na inastahili kupingwa kwa sauti ya juu kabisa.kwani ata kwenye jamii zetu wapo watu wanaoishi katika mitazomo iyo ya imani potofu za kuona watu wenye ulemavu wa ngozi kama ni mikosi.

  • Ndoa za wake wengi

Mzee makwati alikuwa na wake wengi,ambapo aliwaowa kwa sababu sekai alikua hajazaa kwa muda mrefu,pia tunaona katika jamii zetu mwanamke asipozaa wanaume huwa wanaowa wake wengine kwa lengo la kutafuta watoto na kukosa uvumilivu na mke wake wa kwanza.

  • Migogoro

Katika riwaya ya Takadini, mwandishi amebainisha migogoro tofauti tofauti.kwa mfano

  • Mgogoro kati ya sekai na jamii yake.

Jamii ina msimamo kwamba mke anayestahili kuishi na mume ni yule anayazaa tu.Bila ya hivyo, jamii inaamini kuwa, mume anatakiwa amwache mke.kwaiyo hapa ulizuka mgogoro kati ya sekai na jamii yake yote.

  • Mgogoro kati ya Sekai na wake wenza

Kwa sababu ya wivu, wake wenza na Sekai walikuwa hawampendi Sekai kwa sababu alikuwa mke wa kwanza na mzee makwati alikuwa anampenda sababu hao wake wapya walikuwa wanataka mke wa kwanza ambaye Sekai achukiwe na mume wao Makwati.

  • Mgogoro kati ya Takadini na Nhamo.

Nhamo hampendi Takadini kwa kuwa yuko tofauti na watu wote kwa mwonekano.kwa hiyo, hakubali Takadini aje kucheza nao.Anasema:

“Wewe ni sope, sope, sope, umelaaniwa (ukurasa wa 62).

Pia mgogoro wao mwingine ulikuwa katika mgombea Shingai.

  • Shangai na wazazi wake.

Kitendo cha Shingai kuolewa na Takadini na kumkata Nhamo.kilifanya wazazi wake kutofurahishwa na kitendo hiko na kutaka mtoto wao haolewe na Nhamo ambae anatokea familia inayoheshimika pale kijijini.

  • Mgogoro kati ya Makwati na nafsi yake.

Makwati anapopata taarifa kuwa mkewe kazaa mlemavu wa ngozi,anabaki njia panda na kuwa na mgogoro na nafsi yake.

  • Ujumbe.

Ujumbe ni funzo litolewalo na kazi ya fasihi.Mafunzo mengi yametolewa katika riwaya hii.

  • Binadamu wote ni sawa.
  • Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.
  • Ndoa ni makubaliano ya watu wawili.
  • Malezi ya watoto yasimamiwe na wazazi wote.
  • Jamii iachane na mila potofu.
  • Falsafa

Falsafa ya mwandishi inaonekana anaamini kuwa katika maisha kuna changamoto nyingi na changamoto hizo zinaweza kuwa ni mizito sana wakati mwingine,pia anaamini pia binadamu wote ni sawa kwa hiyo tusitengane.

  • Mtazamo /msimamo.

Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani anataka jamii kubadilika kuondoa imani potofu katika jamii zao.

Kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi

Kufaulu

Mwandishi wa kitabu cha Takadini amefaulu kuonyesha kuwa,mila potofu zinaweza kupigwa vita bila kujali ugomvi au msimamo mkali wa jamii.

Pia mwandishi amefaulu kuonyesha kuwa wanawake wanaweza kuwa chanzo cha mabadiliko katika jamii.

Pia mwandishi amefaulu kuonyesha kuwa binadamu wote ni sawa na haistahili kumtenga mtu kutokana ma maumbile yake au muonekano wake.

Kutofaulu.

Mwandishi ameonyesha masuluhisho kwa baadhi ya matatizo yaliyo katika jamii,hata hivyo, masuluhisho hayo yanatia wasiwasi iwapo ndiyo muafaka kwa matatizo yanayohusika.Kwa mfano:

  • Wazazi wa shingai hawapendi binti yao aolewe na albino.Suluhisho lililoonyeshwa ni kwa binti kujipeleka kwa nguvu kwa yule ampendaye.

Kwa hili,ni vigumu kukubali iwapo hilo ni suluhisho sahihi.Je kama yule mchumba wa mwanzo ni mkorofi kama alivyo Nhamo,ataweza kuvumilia jambo hilo? Wazazi wao watakubali kubadilika kwa sababu hiyo? Njia inaweza kuzua mgogoro.

Kuhakiki tamthiliya.

Tamthiliya ni mchezo wa kuigiza ulioandikwa.Tamthiliya huandikwa kwa lengo la kuigizwa jukwaani.

Katika kuhakiki tamthiliya tunaagalia mambo mbalimbali kama yafuatayo

Fani

  • 1.Mtindo

Tamthiliya inafanana na tanzu nyingine lakini,pia ina sura za kipekee.Mambo yanayoipa tamthiliya upekee ni majibizano ya wahusika yaani dayalojia,utendaji na maelekezo ya jukwaa.

  • 2.Muundo

Muundo ni namna kazi ya fasihi ilivyoundwa au ilivyojengwa.Hapa tunaangalia namna tamthiliya ilivyojengwa.Mambo yanayohitajika muhakiki kuyafahamu katika muundo ni:

  • a.Urefu wa tamthiliya
  • b.Sehemu,vitendo na maonyesho
  • c.Msuko au mpangilio wa matukio kuanzia ufunguzi,upeo na mpomoko.
  • d.Mgogoro na ufumbuzi wake
  • e.Maelekezo ya jukwaani.
  • 2.Mandhari

Hii ni eneo ambalo tamthiliya inatendeka yaani tendo la tamthiliya huwa linatendeka jukwaani.Ni muhimu muhakiki afahamu eneo la uigizaji,uangazaji wa jukwaa,maleba(mavazi yanayotumika kwenye kuigizia tamthiliya) na vifaa.

  • 3.Wahusika

Hawa ni viumbe ambao wanatumika kutenda tamthiliya yaani watendaji wa tamthiliya, wazungumzaji na kuendeleza matukio mbalimbali kwenye tamthiliya.Ni muhimu mhakiki afahamu mambo yafuatayo:

  • a.Idadi yao
  • b.Majukumu yao
  • c.Umuhimu wao
  • d.Mavazi yao
  • e.Athari za matendo yao
  • f.Sura, maumbili,majina,tabia na hisia zao
  • g.Matendo yao na yanavyoingiliana
  • h.Nafasi yao katika mgogoro
  • f.Kufanana kwao na watu halisi.
  • 4.Matumizi ya lugha

Mhakiki anapaswa kufahamu yafuatayo

  • a.Lugha ya majabizano baina ya wahusika.
  • b.Aina ya lugha inayotumiwa, kama vile tamathali za semi, methali, misemo na mengineyo.
  • c.Jinsi lugha inavyotumiwa kujenga hali, mtiririko wa matukio, mandhari, wahusika na kadhalika.

MAUDHUI.

  • Mambo ya kuangalia katika tamthiliya katika kuhakiki dhamira ni mawazo ya mwandishi kuhusu mambo yaliyoko katika jamii, kama vile ushirikiano,uvivu,ukabila,rushwa,mapenzi,unyanyasaji,n.k
  • 1.Ujumbe

Ujumbe wa tamthiliya ni mafunzo tunayopata kutoka kwenye tamthiliya husika,kwa mfano ujumbe unaweza kuwa asiyesika la mkuu mguu huota tende au mshika mawili moja humponyoka.

  • 2.Falsafa

Haya ni mawazo fulani ya msanii yanayoonyesha ukweli fulani kuhusu maisha.Ni namna msanii anavyoamini maisha kwa ujumla.kwa mfano falsafa ya msanii inaweza ikawa maisha ni bahati.

  • 3.Migogoro

Hii ni mikinzano mbalimbali katika tamthiliya ambapo hutokea pande mbili kutoelewana juu ya jambo fulani. Hivyo basi kupelekea mtafaruku baina ya watu hao au mtu na mtu, wakati mwingine mgogoro unaweza ukatokea wa nafsi ya ya muhusika mwenyewe na nafsi yake.

Mfano wa uhakiki wa tamthiliya.

Kitabu: Ngoswe penzi kitovu cha uzembe

Mwandishi: Edwin Semzaba

Ufuatao ni uhakiki wa tamthiliya hiyo

  • (a)Muundo

Tamthiliya hii imeandikwa kwa muundo wa moja kwa moja yaani msago.Matukio yake yamepangana kwa mtiririko wa moja kwa moja yaani litoka tukio hili linafuata lingine.

Vilevile mwandishi amepanga kazi yake katika sehemu kuu tano yaaani

  • Kijito
  • Vijito
  • Mto
  • Jito
  • Bahar

•

( b)Wahusika

  • Ngoswe
  • Huyu ni muhusika mkuu
  • Ni kijana ambaye uzembe wake unasababisha karatasi za takwimu kuchomwa moto.
  • Anajihusisha na mapenzi badala ya kuzingatia kazi
  • Ametumiwa na serikali kuhesabu sensa
  • Hana umakini katika kazi
  • Alijihusisha kwenye mapenzi na msichana Mazoea
  • Ni mlevi
  • Hafai kuigwa katika jamii.
  • Mazoea
  • Ni binti wa mzee Mitomingi
  • Alikuwa mpenzi wa Ngoswe
  • Hana elimu
  • Ana nidhamu ya woga
  • Hana msima alikubali kutoroshwa na Ngoswe hali akijua kashatolewa mahari.
  • Ngengemkeni Mitomingi.
  • Ni Baba yake Mazoea
  • Ni mjumbe wa nyumba kumi ambaye mwenyeji wa Ngoswe
  • Ni mume wa wake wawili
  • Alichoma moto karatasi za takwimu ambazo Ngoswe alizidondosha.
  • Mlevi
  • Hajaelimika
  • Anashikilia mila na desturi za kale
  • Mkali sana.
  • Mzee Jimbi
  • Mwanakijiji
  • Hajaelimika kwani hajui hata umri wake
  • Ni mlevi
  • Ana wake wawili
  • Anashikilia mila na desturi za kale
  • Mama Mazoea
  • Mke mkubwa wa Mitomingi
  • Mama yake Mazoea
  • Mlezi wa familia
  • Hapewi nafasi ya kutoa maamuzi katika familia.
  • Mama Inda
  • Mke wa pili mzee Mitomingi
  • Mama yake Huzuni
  • Hapewi nafasi ya kutoa maamuzi
  • Ni mlezi wa familia

©Lugha

Katika tamthiliya hii mwandishi ametumia lugha katika namna mbalimbali.

Kwa mfano

  • Methali

Mwandishi ametumia methali.

Kwa mfano: “penye nia pana njia” uk 22

  • Penye nia pana njia (ukurasa wa 22)
  • Tashbiha

Hutumika kulinganisha vitu au hali mbili au zaidi.kwa mfano

  • Ngoswe anapofikia kijijini anasema,”vumbi jekundu kama ugoro wa subiani”(Ukurasa wa 1).
  • Kutokana na uchovu wa kazi, Mzee Mitomingi anamwambia Ngoswe, “Nikitoka hapa ni kujitupa kitandani kama gogo”.(Ukurasa wa 18).
  • Nahau na misemo
  • Pombe na yeye ni Pete na chanda! (ukurasa wa 14)
  • Hebu keti utupe mawe pangoni. (ukurassa wa 11)
  • Kupiga vibanga (ukurasa wa 3)
  • Mubalagha

Ni kueleza jambo kwa kutia chumvi. Kwa mfano

“Kujibu swali hilo ndio ukachukua mwaka mzima” (ukurasa wa 11).

  • Takriri

Takriri ni kujirudiarudia kwa maneno.

Kwa mfano, Mitomingi anamwambia Ngoswe kwa hasira

  • Nitayochoma ,nitayochoma hakuna maneno.(ukurasa wa 27)
  • Shida shida kitu gani? (ukurasa wa 27).
  • Kejeli / Dhihaka

Kuna matumizi ya kejeli kwenye kazi hii.

Kwa mfano, Mamo Mazoea anamkejeli Ngoswe

Mitomingi: Anatoroshwa na nani?

Mama Mazoea: Masarawili (ukurasa wa 25-26)

Hapa Mama Mazoea amemkejeli Ngoswe kwa kumwita masarawili kwa vile anavaa suruali pana chini.

  • Mtindo

Mwandishi ametumia mtindo wa nafsi ya kwanza,nafsi ya pili,nafsi ya tatu.

Kwa mfano

  • Nafsi ya kwanza

‘Mimi mzima.Samahani mama kwa kukusumbua’ (ukurasa wa 1)

  • Nafsi ya pili

‘Lakini watu wako wana habari’ (ukurasa wa 7).

  • Nafsi ya tatu

‘Na leo afadhali kajiheshimu maana kazoea kupiga vibanga yule mzee na leo mchuzi wenyewe kidogo!’ (Nafsi ya tatu).

  • Mandhari

Mandhari ya tamthiliya hii ametumia mandhari ya kijijini.Mandhari haya yanasadifu vilivyo hali halisi ya maisha ya kijijini.

Maudhui

  • Dhamira

Katika tamthiliya hii mwandishi amebainisha dhamira mbalimbali

  • Suala la Uzembe

Hii dhamira kuu katika tamthiliya hii.Tunamwona mhusika mkuu Ngoswe ambaye alitumwa na serikali kwa ajili ya kuhesabu watu yaani sensa ya watu lakini akashiriki mapenzi na Mazoea na kujikita kwenye ulevi mpaka kupoteza baadhi ya karatasi za kuhesabia watu.kupelekea Mzee Mitomingi kuzichoma moto karatasi hizo.

Katika jamii yetu suala la uzembe linajitokeza kuna baadhi ya watendaji wa serikali yetu wanajisahau na kujikita katika mapenzi na ulevi na kusahau majukumu yao.

  • Suala la Mapenzi

Mwandishi amezungumzia suala la mapenzi, tunaona Ngoswe na Mazoea wanaingia katika mapenzi mazito mpaka kutokea Ngoswe kutaka kumtorosha Mazoea kutoka kijijini kwao kwenda mjini japo hawakufanikiwa.Tunaona mapenzi ya namna hii hujitokeza katika jamii zetu wapo watu wanajitoa muhanga na wapenzi wao kisa mapenzi wapo tayari kugombana na familia zao kisa mapenzi.

  • Suala la Umaskini

Mwandishi ameonesha hali ya umaskini jinsi ilivyokithiri pale kijijini kiasi kwamba mgeni alipofika pale kijijini Mzee Mitomingi anamwambia Ngoswe akalale kibandani (Ukurasa 3). Vilevile katika jamii zetu hali ya umaskini ni jambo lililokithiri sana watu wengi wanaishi maisha duni hali inayofanya wengine kukosa kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

  • Ushirikina na Imani potofu.

Mwandishi amejaribu kuonyesha imani za kishirikina kwani wanakijiji wanaamini kuhesabiwa ni uchawi, mfano Mama mjane anaamini kuhesabiwa ni uchawi (ukurasa wa14).Pia imani za kishirikina katika jamii zetu ni jambo kubwa na wanajamii wengi wanaamini katika ushirikina kwani ata wakiumwa kidogo wanaamini wamerogwa na kukimbilia kwa waganga na kupelekea baadhi yao kupoteza maisha.

  • Suala la Ulevi

Ni hali iliyojitikeza katika tamthiliya hii kwani tunamuona Ngoswe analewa kiasi cha kusahau majukumu yake, pia pale kijijini wazee wengi ni walevi kwan Mzee Mitomingi ni mlevi wa kutupwa.Pia hali ya ulevi inajitokeza katika jamii zetu watu wengi husahau majukumu yao,kwa sababu ya ulevi.

  • Huduma duni za jamii

Huduma kama vile elimu na matibabu ni duni. Kwa mfano, Ngoswe anapomuuliza Mama Mjane iwapo wanawe wanasoma, anajibiwa “Hapana. Shule i mbali sana” (Ukurasa wa 16).

Pia huduma za kijamii katika jamii zetu za kiafrika ni duni mnoo kiasi kwamba hupelekea vifo vya watu kukosa huduma za matibabu, pia kuna idadi kubwa ya wajinga kutokana kundi kubwa la watu wamekosa elimu.

  • Ujumbe

Ujumbe tunaopata katika tamthiliya hii ni kwamba uzembe katika kazi,ulevi na mapenzi yasiyofuata utaratibu ni chanzo cha kuharibu utendaji wa kazi. Hivyo yatupasa kuwa makini na kazi na kutochanganya mambo mawili kwa wakati mmoja,yaani mtaka yote kwa pupa hukosa yote. Na tamaa ilimshinda fisi, hivyo umakini ni muhimu katika kazi hususani kila kazi yatupaswa kuwa makini.

  • Falsafa

Falsafa ya mwandishi anaamini kuwa kuishi kijamaa ndio chanzo cha maisha bora katika jamii. Anaamini ujamaa ndio utakaomaliza matatizo katika jamii zetu.

  • Migogoro

Kuna migogoro mbalimbali iliyojitokeza ndani ya tamthiliya hii

Kwa mfano

  • Mgogoro kati ya Ngoswe na Mzee Mitomingi.

Mzee Mitomingi anakasirishwa na kitendo cha Ngoswe kutaka kumtorosha binti yake. Kwahiyo hapa mgogoro ulikua katika ya Mitomingi na Ngoswe.(Ukurasa wa 27).

Matokeo yake, Mitomingi anachoma moto karatasi za takwimu za Ngoswe kwa hasira.

  • Mgogoro kati ya Mazoea na Baba yake Mitomingi;

Mgogoro huu unatokana na kwamba Mazoea alitaka kutoroshwa na Ngoswe wakati alitaka kuolewa na mtu mwingine. Kitendo hiki kilimchukiza Mzee Mitomingi na kumgombeza mtoto wake Mazoea.

  • Mgogoro wa Ngoswe na Serikali

Kwa sababu Ngoswe kushindwa kutekeleza jukumu alilokabidhiwa na serikali kutokana na uzembe kazini.Ngoswe anaingia kwenye matatizo makubwa na serikali mpaka kumfungulia mashitaka mahakamani.

  • Mgogoro kati ya Mitomingi na familia yake

Mzee Mitomingi anakasirishwa na kitendo cha wake zake kukaa kimya hadi mazoea anatoroshwa na Ngoswe, wake zake wanakiri kuwa waliona dalili za mapenzi kati ya Ngoswe na Mazoea .Hii ilipelekea mzee Mitomingi kuwagombeza wake zake.(Ukurasa 26).

Kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi.

Kufaulu

Mwandishhi amefaulu kuonyesha kwamba uzembe kazini ni chanzo cha matatizo hata kupelekea kufukuzwa kazi. Jambo kama mapenzi ni vizuri kufuata utaratibu wake na lisipofuata utaratibu wake inaweza kuweza kuwa chanzo cha matatizo katika jamii na kupelekea kuharibu kazi.

Kutofaulu

Msanii huyu hakufanikiwa kuonesha masuluhisho ya matatizo katika tamthiliya hii mfano umaskini, ulevi, huduma duni za kijamii, hazikuoneshwa masuluhisho yake. Kwa hiyo amefeli kuonesha jinsi gani umaskini, ulevi, huduma mbaya za kijamii zinavyoweza kutatuliwa.

Kuhakiki ushairi

Maana ya ushairi

Ushairi ni utanzu wa fasihi unaoeleza mawazo mazito kuhusu jamii. Mawazo hayo huwekwa katika lugha ya mkato na urembo. Ushairi, pia hutumia lugha ya picha.

Uchambuzi wa mashairi

Katika uchambuzi wa mashairi tunaangalia mambo yafuatayo

Fani

  • 1.Wahusika

Kuna baadhi ya mashairi huwa yana wahusika, japo mara nyingi msemaji wa shairi huwa ni mshairi mwenyewe.

  • 2.Lugha
  • a.Kuna lugha ya ishara?
  • b.Je mshairi ametumia tamathali za semi, kama vile sitiari, tashihidi, mubalagha na kadhalika.
  • c.Je mshairi ametumia idhini ya mashairi yaani washairi wana uhuru wa kuvunja sheria za lugha kwa lengo la kuleta urari wa vina na mizani.
  • d.Je mshairi ametumia mbinu gani nyingine za lugha?
  • 3.Muundo

Muundo wa shairi unategemea iwapo shairi linalohusika ni la kimapokea au ni la kisasa.

  • Mashairi ya kimapokeo ni mshairi ni mashairi ambayo yanazingatia kanuni maalum. Kanuni hizo ni uzingatiaji wa urari wa vina na mizani,utoshelevu wa beti,pia kila ubeti huwa na idadi ileile ya mishororo (mistari). Yaani mashairi ya kimapokeo ndio mashairi yanayofuata kanuni zote za ushairi tofauti na maishairi ya kisasa.

Idadi ya mishororo huweza kutofautisha kati ya aina mbalimbali za maishairi hivyo kuibua miundo mbalimbali:

  • a.Tathnia - shairi lenye mistari miwili katika ubeti.
  • b.Tathlitha - shairi lenye mistari mitatu.
  • c.Tarbia - shairi lenye mistari minne.
  • d.Takhmisa - shairi lenye mistari mitano.

Asilimia kubwa ya mashairi ya kitanzania yanatumia mashairi yenye mistari minne (Tarbia).

  • Katika mashairi haya mstari wa kwanza katika ubeti huitwa mwanzo
  • Mshororo wa pili huitwa ni mloto.
  • Mshororo wa tatu ni mleo.
  • Mstari wa nne huitwa kituo.

Mshororo mmoja wenye mizani nane huwa na vipande viwili kila mmoja

  • Ukwapi ni kipande cha kwanza
  • Uteo ni kpande cha pili.

Mshororo mzima mara nyingi huwa na mizani 16. Silabi ya mwisho katika kila mshororo huitwa kina.

  • 4.Mtindo

Ni ufundi anaotumia msanii au mwandishi wa mashairi kumtofautisha yeye na waandishi au wasanii wengine. Kwahiyo mtindo katika ushairi unaonyesha namna kazi ya Sanaa ilivyofikishwa kwa jamii au hadhira husika.

MAUDHUI.

  • 1.Dhamira

Tunachoangalia katika uchambuzi wa dhamira ni mawazo ya mwandishi juu ya jamii,yaani mambo yaliyoko katika jamii zetu. Kwa mfano umasikini, ulevi, rushwa,unyanyasaji, uroho wa madaraka,imani za kishirikina , mapenzi n.k.

  • 2.Ujumbe

Ujumbe ni funzo tunalolipata kutoka kwenye ushairi. Kwa mfano ujumbe unaweza ukawa “haba na haba hujaza kibaba”

  • 3.Falsafa

Falsafa ni mawazo anayoyaamini msanii au mshairi kuwa ndio ukweli kuhusu maisha kwa ujumla. Falsafa hujitokeza zaidi baada ya kusoma kazi kadhaa za msanii. Kwa mfano falsafa ya mshairi inaweza ikawa kilimo ndio chanzo cha maendeleo kwa kila mtu.

Mfano wa uhakiki wa mashairi

Shairi: Wasaka Tonge

Mshairi: Mohamed .S. khatibu

Utangulizi

Diwani au mashairi haya ya wasakatonge ni diwani ambayo mashairi yake yameandikwa kwa idadi kubwa ambapo yapo takribani mishairi sitini na moja. Kutokana na kutaka kupanua uelewa wa wanafunzi na kutengeneza mazingira wanafunzi waweze kujitegemea, tumefanya uchambuzi wa maishairi machache, ambapo mwanafunzi anaweza kuyapitia na kupata uelewa juu ya mashairi yaliyobaki. Ni vyema mwanafunzi akachambua mashairi yote ili apate uelewa zaidi.

  1. Wasakatonge
  1. Wasakatonge na juakali

Wabeba zege ya maroshani,

Ni msukuma mkokoteni,

Pia makuli bandarini,

Ni wachimbaji wa migodini,

Lakini maisha yao chini.

  1. Juakali na wasakatonge

Wao ni manamba mashambani,

Ni wachapa kazi viwandani,

Mayaya na madobi wa nyumbani,

Ni matopasi wa majaani,

Lakini bado ni masikini.

  1. Wasakaatonge na juakali

Wao huweka serikalini,

Wanasiasa madarakani,

Dola ikawa mikononi,

Wachaguliwa wa ikuluni,

Lakini wachaguaji duni.

  1. Juakali na wasakatonge

Wao ni wengi ulimwenguni,

Tabaka lisilo ahueni,

Sikuzote wako matesoni,

Ziada ya pato hawaoni,

Lakini watakomboka lini?

Fani

1.Mtindo

Shairi la wasakatonge ni shairi la kisasa. Mpangilio wake unaonesha kuwa shairi hili ni huru, halifungamani na kanuni za kimapokeo.

2.Muundo

Idadi ya mistari katika shairi hili ni mistari sita (6). Hivyo muundo wake ni Tarsidisa.

Matumizi ya Tamathali za Semi

3.Taswira

Mshairi ametumia taswira tofauti katika kujenga picha kwa wasomaji

Juakali - imetumika kuonyesha hali ngumu ya maisha wanayoishi watu wa tabaka la chini.

Wasakatonge - imetumika kuonyesha taswira ya watu wenye hali ngumu kimaisha,hasa kupata huduma za kijamii hususani chakula,maradhi na makazi.

Mbinu nyingine za kisanaa

Dhamira

1.Umasikini: ni hali ya kushindwa kukidhi mahitaji muhimu ya maisha mfano chakula, maradhi na makazi. Mshairi amelithibitisha hilo anaposema:

“…Ni matopasi wa majaani,

Lakini bado ni masikini…”

2.Utabaka: Kundi la watu katika jamii linalojitofautisha na kundi jingine kwa misingi ya kiuchumi na kielimu. Mshairi anaonyesha kwamba katika jamii yetu kuna utabaka. Anaenda mbali zaidi na kuonesha kwamba wasakatonge ni watu wa tabaka la chini. Anaposema:

“…Wao ni wengi ulimwenguni,

Tabaka lisilo ahueni…”

3.Unyonyaji: ni hali au tabia ya mtu au kikundi kupokea mapato makubwa bila ya kufanya kazi au kwa kufanya kazi kidogo. Mshairi katika ubeti wa kwanza anonesha kuwa watu wa tabaka la chini hufanya kazi nzio na za nguvu kunufaisha wenye pesa lakini wao siku zote hubaki masikini.

“…ni wachimbaji wa migodini,

Lakini maisha yao chini…”

  1. Wasodhambi
  2. Wasodhambi!

Wako wapi? Ni wangapi?

Nchi zipi? Chao kipi?

Haki ipi? Nakuwa vipi?

Nauona,

Unafiki.

  1. Wavilemba!

Wavilemba, na majoho, tasibihi,

Wajigamba, safi roho, ni kebehi,

Wanotenda,

Unafiki.

  1. Warozari!

Misalaba, na majuba, na hotuba,

Nyingi toba, zenye hiba, na haiba,

Mambo yao,

Unafiki.

Fani

  • 1.Mtindo

Shairi la wasodhambi ni shairi la kisasa. Mpangilio wake unaonesha kuwa shairi hii ni huru, halifungwi na kanuni za kimapokeo.

  • 2.Muundo

Muundo katika ushairi huzingatia idadi ya mistari katika shairi. Idadi ya mistari ni mitano (5) hivyo muundo wake ni takhmisa.

  • 3.Lugha

Msanii au mshairi ametumia lugha nyepesi na rahisi ambayo inaweza kufahamika na kila mtu. Pia mshairi ametumia matumizi mbalimbali ya tamathali ya semi kama ifuatavyo:

  • a.Tashibiha

Maneno yanayotumiwa kuunganisa hali au vitu viwili kuumba taswira fulani.

Misalaba na majuba

Wa vilemba na majoho

Ametumia kuunganisha maneno hayo kwa kuonesha watu wenye maadili.

  • b.Matumizi ya kebehi na kejeli/dhihaka.

Kuna matumizi ya kejeli au dhihaka katika shairi hili pale mshairi anaposema

Wavilemba!

Wavilemba, na majoho, tasibihi,

Wajigamba, safi roho, ni kebehi,

Wanotenda,

Unafiki.

Msanii au mshairi anaonesha kuwakebehi au kuwadhihaki watu wanaojifanya wasafi kumbe wachafu.

  • Taswira

Mshairi ametumia taswira zifuatazo katika shairi hili ili kujenga picha kwa wasomaji

Wasodhambi – muunganiko wa maneno mawili: wasio na dhambi.

Wavilemba – watu wenye maadili

Majoho – watu wasomi

Warozari – wakristu safi

Misaraba – wakristu safi

Majuba – waislamu safi

Tasibihi – waislamu safi

Hotuba – wanasiasa/ wasomi

Dhamira

Shairi hili lina dhamira moja kuu

Unafiki: mshairi anaonesha kuwa baadhi ya watu wanaoonekana watakatifu mbele za macho ya jamii huwa ni wanafiki kwa kuwa wanafanya dhambi kama watu wengine. Kwa mfano katika ubeti wa pili mshairi anasema:

“…Wajigamba,safi roho, ni kebehi,

Wanotenda,

Unafiki.”

Mshairi anatumia taswira kama; waviremba, majoho, tasibihi na majuba ili kuwasilisha watu wema. Lakini katika uhalisia watu hawa wanamatendo ya dhambi kama watu wengine.

  1. Hatuna kauli
  2. Hatuna sisi kauli,

Ni kwa yetu sisi maduhuli,

Si umma si serikali.

  1. Mavuno yetu shambani,

Madini ya aridhini,

Ulaya bei ni duni.

  1. Vitu vyao viwandani,

Madawa pia mashini,

Bei zake za thamani.

  1. Maagizo tunapewa,

Mipango tunapangiwa,

Na amri tunatolewa

  1. Sera zote sio zetu,

Zimeletwa huku kwetu

Hazina faida katu.

  1. Twapewa yake mitaji

Tuwe wasimamiaji

Pia watekelezaji

  1. Tunatumia nguvu zetu

Bila kupata kitu

Chenye na faida kwetu.

  1. Hakika ni uonevu,

Kwa kujifanya werevu

Wenye mbinu za mabavu.

Fani

  • 1.Muundo

Shairi la hatuna kauli ni shairi la kisasa, mpangilio wake haufungwi na kaida za kimapokeo.

Muundo: shairi hili lina, muumdo wa tathilitha; idadi ya mistari ni mitatu (3).

  • 2.Mtindo

Katika shairi hili mshairi ametumia mtindo wa nafsi ya kwanza wingi kwa mfano anasema katika ubeti wa kwanza

“Hatuna sisi kauli

Ni kwa yetu maduhuli”

  • 3.Lugha

Mwandishi wa shairi ametumia lugha rahisi na inayoeleweka,yaani ya moja kwa moja na isiyoficha dhamira yake, na kufikisha ujumbe moja kwa moja kwa jamii au hadhira.

Pia katika matumizi haya ya lugha mshairi ametumia tamathali za semi tofauti tofauti kama ifuatavyo:

  • Taswira

Taswira zilizotumika katika shairi hili hasa ni jina la shairi; kimsingi jina hili linasimamia dhana kwamba nchi za kiafrika bado ziko chini ya ukoloni.

Dhamira

1.Unyonyaji: ni hali au tabia ya nchi au kikundi cha watu kupokea mapato makubwa bila ya kufanya kazi au kwa kufanya kazi kidogo. Mshairi anaonesha dhamira hii katika ubeti wa pili anapojadili juu ya bei za mazao na madini yanayotoka katika nchi zetu katika soko la dunia. Anasema:

“Mavuno yetu shambani,

Madini ya aridhini,

Ulaya bei ni duni”

2.Ukandamizaji: ni hali au namna ambayo kundi fulani la watu hunyima haki wananchi wengine katika mambo ya kisiasa na uchumi. Dhana ya ukandamizaji imejadiliwa katika shairi hili, mshairi anafafanua namna bidhaa kutoka nchi za magharibi zinavyouzwa kwa bei ghali ukilinganisha na bidhaa kutokakwetu Africa. Katika ubati wa tatu, mshairi anasema:

“Vitu vyao viwandani,

Madawa pia mashini,

Bei zake za thamani”

3.Ukoloni mamboleo: ni namna ya utawala wa chi za kibepari ya kuathiri na kuamua juu ya uchumi na siasa ya nchi zinazoendelea kwa maslahi yao. Mshairi anagusia suala hili anapojadili juu ya mataifa ya ulaya na jinsi yanavyozipangia nchi za kiafrika sera na utekelezaji wake. Katika ubeti wa nne mshairi anasema:

“Maagizo tunapewa,

Mipango tunapangiwa,

Na amri tunatolewa”

  • Ujumbe

Ujembe tunaopata katika shairi hili ni kuwa,uhusianao uliopo kati ya Afrika na ulaya haustahili kuendelea kama ulivyo,maana ukandamizaji wa bara la Afrika bado unaendelea na kunufaisha mataifa makubwa tu.

  • Falsafa

Mwandishi anaamini kuwa mwanadamu mwenye nguvu hawezi kamwe kumjali na kumsaidia maskini na mtu dhaifu. Hii inatokana na uroho na uchu wa rasilimali na utajiri.

  • Msimamo

Msimamo wa mwandishi anaonesha kuwa lazima kuwa na usawa kati ya nchi za Afrika na ulaya ili kuzifanya nchi za kiafrika kupiga hatua katika maendeleo. Lakini tukikosa usawa nchi za kiafrika zitakuwa bado ziko nyuma kimaendeleo.

  • Kufaulu

Mshairi amefaulu kuonyesha bayana ukandamizaji wa mataifa makubwa kwa nchi ndogo hususani nchi za kiafrika. Kwani mshairi ametumia lugha rahisi nay a moja kwa moja na kufanya watu waelewe nini anachokimaanisha.

  1. Mwanamke
  2. Namwona yu shambani,

Na jembe mikononi,

Analima

Mwanamama,

Mavuno si yake,

Ni ya mume wake.

  1. Namwona viwandani,

Pia maofisini,

Yu kazini,

Hamkani,

Anabaguliwa,

Na anonewa.

  1. Namwona yu nyumbani,

Mpishi wa jikoni,

Yaya yeye,

Dobi yeye,

Hakuna malipo

Likizo haipo.

  1. Namwona kitandani,

Yu uchi maungoni,

Ni mrembo,

Kama chombo,

Chenye ushawishi,

Mzima utashi.

  1. Namwona mkekani,

Yuwamo uzazini,

Apumua

Augua,

Kilio cha kite,

Cha mpiga pute.

  1. Kwa nini mwanamke,

Ni yeye peke yake,

Anyimwaye,

Heshimaye,

Haki anakosa,

Kwa kweli ni kosa.

Fani

  • Mtindo

Shairi la Mwanamke ni shairi la kisasa, mpangilio wake na idadi ya mistari havifungwi na kaida za kimapokeo.

  • Muundo
  • Idadi ya mistari katika shairi hili ni mistari sita (6). Hivyo muundo wake ni Tarsidisa.
  • Lugha

Katika shairi hili mwandishi ametumia lugha nyepesi na rahisi,pia lugha yenye lugha za ushairi ndani yake. Pia kuna matumizi ya tamathali za semi kama zifuatazo:

Jaribu quiz ya KiswahiliMaswali 31