Kiswahili · Kidato 3

Ngeli za nomino

Dakika 5 za kusoma ·

Yaliyomo

Maana ya ngeli za nomino

Ngeli maana yake ni kundi au aina. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika mpangilio au kupanga nomino katika makundi yenye nomino zinazofanana.

Mfano

Maneno mtoto na mjomba yako kwenye ngeli moja, kwa sababu katika umoja yote yanaanza na m huku vitenzi vyake vikianza na a, pia katika wingi yanaanza na wa huku vitenzi vyao vikianza na wa.

Aina za Ngeli za Nomino

Nomino zote za lugha ya Kiswahili zinaweza kugawanyika katika makundi au ngeli mbalimbali.

Njia mojawapo ni kutumia kigezo cha upatanisho wa kisarufi.

Njia hii inaangalia jinsi nomino inavyopatana na kiambishi awali cha kitenzi katika tungo. Tazama sentensi zifuatazo.

Mfano

Mtoto anaimba

Mtoto wanaimba

Umoja Wingi

Mtoto amekimbia Watoto wamekimbia

Mjomba amerudi Wajomba wamerudi

Chama chao kimeshinda Vyama vyao vimeshinda

Kiti kimepotea Viti vimepotea

.

Sentensi ya kwanza ni sahihi lakini ya pili si sahihi.

Kwa kuzingatia kigezo hiki cha upatanisho wa kisarufi, kuna ngeli tisa za nomino[vitabu vingine 10]. Ngeli hizo ni;

  1. A-wa
  2. U-ya
  3. U-zi
  4. U-I
  5. Li-ya
  6. Ki-vi
  7. Ku
  8. i-zi
  9. Pa/mu/ku
  10. U. [baadhi ya vitabu vinaitaja]

i] Ngeli ya a-wa

Ngeli hii inajumuisha majina ya viumbe hai kama vile watu, wadudu, ndege, na wanyama.

Kwa mfano

Umoja Wingi

Mwizi amekamatwa Wezi wamekamatwa

Kambare anaogelea Kambare wanaogelea

Kunguru anapaa Kunguru wanapaa

Kinyonga anapita Vinyonga wanapita

[ii] Ngeli ya u-ya

Ngeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u- katika umoja na ma katika wingi.

Kwa mfano. Ugonjwa, ugomvi, ulezi, udanganyifu

Umoja Wingi

Ulezi umemshinda Malezi yamemshinda

Unyoya unapepea Manyoya yanapepea

Uuaji umekithiri Mauaji yamekithiri

Ugonjwa umezuka Magonjwa yamezuka

[iii] Ngeli ya u-zi

Katika ngeli hii kuna majina yenye viambishi awali u- na z- katika wingi

Kwa mfano

Umoja Wingi

Ukuta umeanguka Kuta zimeanguka

Ungo umetoboka Nyungo zimetoboka

Wimbo umenivutia nyimbo zimenivutia

Wembe umenikata Nyembe zimenikata

[iv] Li-ya

Katika ngeli hii, huingia majina ambayo yana kiambishi awali, li- katika umoja na ya- katika wingi.

Mfano, shirika, gunia, jani, jabali, kaa, embe, chungwa, ziwa, jicho, jiwe, jino, shati gauni nk.

Umoja Wingi

Shirika limefirisika, Mashirika yamefirisika

Jani limedondoka Majani yamedondoka.

Embe limeiva Maembe yameiva

Tunda limeoza Matunda yameoza

[v] Ngeli ya u-i

Katika ngeli hii yanaingia majina ya baadhi ya sehemu za mwili, miti nk.

Mfano, mkono, mguu, mpapai, mwarobaini, mninga, mbuyu, mgongo,

Umoja Wingi

Mkono umeumia Mikono imeumia

Mgongo unauma Migongo inauma

Mninga una mbao imara Mininga ina mbao imara

Mguu umevunjika Miguu imevunjika

[vi] Ngeli ya ki-vi

Majina mengi katika ngeli hii ni ya vitu visivyo na uhai. Hivi ni vitu ambavyo huambatana na vitenzi ambavyo vina viambishi awali ki- katika umoja na vi- katika wingi

Mfano. Kitanda, kiti, kisima, chumba, kibarua, kisu, kilima, chungu nk.

Umoja Wingi

Kitanda kina kunguni Vitanda vina kungunii

Kisima kimekauka Visima vimekauka

Chumba kimeandaliwa Vyumba vimeandaliwa

Kiti kimepotea viti vimepotea

[vii] Ngeli ya ku-

Katika ngeli hii yanaingia majina yote yanayotokana na kunominishwa kwa vitenzi. Kwa mfano, kulima ni jina lililotokana na kunominisha kitenzi lima.

Mfano. Kuimba, kulima, kucheza, kufeli, kuongea

Umoja

Kudanganya kumemponza

Kusoma kunasaidia

Kuimba kumemwokoa

Kulima kumempunguzia umaskini.

[viii] i-zi

Ngeli hii hujumuisha majina ambayo hayabadiliki umbo katika umoja na katika wingi.

Mfano kazi, afya, salamu, nyumba, njia,

Umoja Wingi

Kazi imemalizika Kazi zimemalizika

Nyumba imeungua Nyumba zimeungua

Salamu imefika Salamu zimefika

Njia imefungwa Njia zimefungwa

Afya imeboreka Afya zimeboreka

[ix] Ngeli ya pa/mu/ku

Katika ngeli hii yanaingia majina yanayoonesha mahali.

Mahali hapa palikuwa pazuri.

Ndani kumepambwa sana

Mahali kule kunauzwa

Mahali mule muna harufu mbaya.

[x] Ngeli ya u.

Yanaingia majina mengi yanayoanza na kiambishi awali cha u katika kitenzi.

Mfano uongo, ugali, unga, uji, uchokozi, ukiritimba, ulimbwende, uvivu, uroho

Ulimbwende unamfaa

Unga umeisha

Ugali umeiva

Uongo umeenea.

Ulaji [wa mali ya umma] umekithiri.

Upatanisho Wa Kisarufi

Upatanisho wa kisarufi ni hali ya viambishi vya maneno ya ndani ya tungo kukubaliana na kushikamana ili kuleta maana iliyokusudiwa.Upatanisho wa kisarufi unaweza kuonekana kati ya vipashio mbalimbali vya tungo; Mfano

a)Watu iko mingi

Tunaposoma tungo au kusikia tungo iyo hapo juu, tunatambua wazi kuwa ina makosa .hivyo basi tunaweza kuingiza vipashio sahihi pale kwenye makosa.

Yaani: Watu wako wengi

  1. Mfano: unyasi umeota

Nyasi zimeota.

Hivyo basi utaratibu wa viambishi wa-,wa-, na we kwenye sentensi ya kwanza na viambishi nya, na zi kwenye sentensi ya pili kukubaliana kwa jinsi hii ndiyo unaoitwa upatanisho wa kisarufi.

Upatanisho wa kisarufi unaweza kuonekana kati ya vipashio mbali mbali vya tungo.

Mfano

  • Nomino na kitenzi

Kwa mfano

  • Kiti kimevunjika __________viti vimevunjika
  • Jani limedondoka ________Majani yamedondoka
  • Mwezi umepita _________Miezi imepita
  • Kibarua kimepatikana_____Vibarua vimepatikana
  • Unyasi umeota ________ Nyasi zimeota
  • Nomino na Kivumishi

Kwa mfano

  • Kijana mrefu ______vijana warefu.
  • Mkono mfupi ______Mikono mifupi.
  • Kiazi kitamu ______viazi vitamu.
  • Kiti cheupe _______viti vyeupe.
  • Kiwakilishi na kivumishi

Kwa mfano

  • Kile cheusi ______vile vyeusi
  • Huyu mnene _____ Hawa wanen e
  • kiwakilishi na kitenzi

Kwa mfano

  • Huyo anakuja _______Hao wanakuja
  • Hicho kinaanguka_____Hivyo vinaanguka
  • Hili silitaki ________Haya siyataki
  • Nomino na mzizi wa amba

Kwa mfano

  • Mtu ambaye _____watu ambao
  • Kiti ambacho _____viti ambavyo
  • Gari ambalo _____Magari ambayo
  • Ukuta ambao _____kuta ambazo
  • Njia ambayo _____Njia ambazo
  • Nomino na kirejeshi

Kwa mfano

  • Kitanda kilichovunjika_____vitanda vilivyovunjika
  • Mnazi uliokatwa______ minazi iliyokatwa
  • Mtoto aliyesafiri ______ watoto waliosafiri

•

Maswali

  1. Nini maana ya ngeli za nomino?

2.Yapange maneno yafuatayo katika ngeli zake

Kuku,mkono,kiti,uso,upepo,wimbo na mtoto.

3.Eleza maana ya upatanisho wa kisarufi.

4.Sentensi zifuatazo zina makosa,kwa kutumia kigezo cha upatanisho wa kisarufi ziandike kwa usahihi.

a.Watoto amekuja.

b.Mbuzi zimekufa

c.Wanafunzi amefeli

5.Tunga sentensi moja kuonyesha upatanisho wa kisarufi kati ya

a.Kitenzi na kielezi

b.Nomino na kivumishi

c.Kiwakilishi na kivumishi

Jaribu quiz ya KiswahiliMaswali 31