Kiswahili · Kidato 5

Matumizi ya Sarufi

Dakika 15 za kusoma ·

Yaliyomo

Sarufi ni utaratibu wa sheria au kanuni zinazowezesha muundo wa lugha

kukubalika. Matawi ya Sarufi

  1. Sarufi matamshi (fonolojia)

Tawi hili la sarufi huhusu utaratibu wa mpangilio wa vitamkwa katika maneno

ya lugha. Sauti zinazotolewa katika lugha ni irabu na konsonanti. Sauti hizi

zinapotumiaka katika maneno ya lugha huitwa fonimu. Fonimu ni kipashio kidogo cha kifonolojia kinachobadili maana ya neno. Hivyo, tawi hili la fonolojia, limejikita katika matamshi ya maneno. 2. Sarufi maana (semantiki)

Tawi hili la sarufi hujihusisha na maana mbalimbali katika tungo. Maneno

hubeba maana fulani, hivyo katika tawi hili, tunaweza kubaini maana yake. Kwa mfano: Maana ya mbuzi ni mnyama afugwaye na aliyefanana na swala. 3. Sarufi miundo (sintaksia)

Tawi hili hujihusisha na mpangilio wa maneno katika kutengeneza sentensi. Ili

kupata sentensi, ni lazima kufuata mpangilio sahihi vinginevyo sentensi hiyo

haitaeleweka wala kukubalika kwa watumiaji wa lugha. Kwa mfano: Mtoto Mzuri amecheza ngoma na sasa anakwenda kulala. Sentensi hiyo imefuata muundo sahihi na hiyo inaifanya ieleweke. 4. Sarufi maumbo (mofolojia)

Hili ni tawi la sarufi ambalo linajihusisha na maneno na aina za maneno. Pia

tawi hili huyatambulisha maumbo ya umoja, wingi n.k

Kwa mfano: mtu - watu

Katika mfano huo, m- ni umbo la umoja na wa- ni umbo la wingi. Matumizi ya mofimu

Mofimu ni kipashio kidogo chenye maana ya kisarufia au kileksika. Kipashio

hicho kinaweza kuwa sehemu ya neno au neno zima. Mofimu zenye maana ya kileksika ni zile ambazo huwa haziongezwi kipashio

kingine, kwa mfano: Baba, Mama, fikiri, bora.

Mofimu zenye maana ya kisarufi ni zile ambazo huambatana na vipashio

vinginie ili viweze kuleta maana. Kwa mfano: m-toto, u-so-mi. Mzizi wa neno ni sehemu ya neno inayobaki baada ya kuondoa viambishi

vyote. Kwa mfano: -chez- Dhima za mofimu

1.Kuonesha nafsi

Kwa mfano: Ninasoma - nafsi ya kwanza umoja

2.Kuonesha njeo

Alisoma - wakati uliopita

3.Kuwakilisha hali

Analima - hali ya kuendelea kwa tendo

Hulima - hali ya mazoea

4.Kuonesha udogo wa nomino

Kipaka

5.Kuonesha ukubwa wa nomino

Jitu

6.Kuonesha urejeshi wa mtendwa na mtendewa

Anaupanda - mtendwa

Aliniandika - mtendewa

7.Kuonesha kujirejelea

Ninajisomea

8.Kuonesha uyakinishi na ukanushi

Ninasoma - sisomi

9.Kuonesha kauli mbalimbali

Limwa - kauli ya kutendwa

10.Kuzalisha maneno ya lugha

Maneno mapya hupatikana kwa kubadili mofimu tegemezi. Kwa mfano: katika

mzizi lim: tunapata maneno: analima, anayelima, analimisha, analimika, analimia n.k

Viambishi

Viambishi ni mofimu zinazowekwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha

muundo wa neno hilo. Katika lugha ya Kiswahili, viambishi vinaweza kuwekwa

kabla na baada ya mzizi wa neno. Kwa mfano katika neno ‘anacheza’ kuna

viambishi awali na tamati navyo tutavifahamu baada ya kutazama aina za

viambishi. Aina za viambishi

  1. Viambishi awali

Hivi ni viambishi ambavyo hutokea kabla ya mzizi wa neno. Viambishi hivi

huweza kuwa vya: idadi, ukubwa wa nomino, udogo wa nomino, ukanushi, njeo n.k

Katika neno Wa-na-lim-a, wa, na , na ni viambishi awali. 2. Viambishi tamati

Hivi ni viambishi ambavyo huwekwa baada ya mzizi wa neno. Kwa mfano: Shind-an-a, an na a, ni viambishi tamati. Kauli za kiswahili

Katika lugha ya Kiswahili, kauli huhusisha uhusiano uliopo baina ya kiima na

kitenzi. Mnyambuliko wa vitenzi huzalisha kauli tofauti tofauti kama hizi

zifuatazo

Kauli ya kutenda

  • piga
  • cheza

Kauli ya kutendwa

  • pigwa
  • somwa

Kauli ya kutendewa

  • katiwa
  • rukiwa

Kauli ya kutendeka

  • fanyika
  • shukika

Kauli ya kutendea

  • pigia
  • lalia

Kauli ya kutendesha

  • imbisha
  • limisha

Kauli ya kutendana

  • pendana
  • katana

Kauli ya kutendua

  • tegua
  • pangua

Kauli ya kutendama

Kauli hii hurejelea hali ambayo watu au vitu hunaswa mahali pamoja kwa

muda na kwa namna ya msuguano. - Gandama

  • Fichama

Kauli ya kutendeana

  • Chezeana
  • Limiana

Kauli ya kutendeshwa

  • Limishwa
  • Chemshwa

Hizo ni baadhi tu ya kauli za lugha ya Kiswahili. Ngeli za nomino

Ngeli ni utaratibu wa kuweka nomino katika makundi yanayofanana au

yanayowiana. Nomino za Kiswahili zinaweza kugawanywa katika makundi

mbalimbali. Baadhi ya wanaisimu wamezigawanya nomino katika makundi 16

na wengine makundi 9 na wengine makundi 18.

Ngeli kwa mtazamo wa Kimapokeo/maumbo

Hiki ni kigezo kikongwe zaidi kilichotumiwa na wanasarufi mapokeo, miongoni

mwao akiwa Meinhof ambao waliyaainisha majina kulingana na maumbo ya

viambishi awali vya nomino. Nomino zote zote zilizokuwa na viambishi awali

vinavyofanana viliwekwa katika kundi moja na kufanya ngeli moja. Kutokana

na kigezo hiki kuna ngeli 18 za kiswahili. Ngeli Sifa za nomino za ngeli Mfano wa nomino za

ngeli

  1. -Mu- 2. -Wa-
  2. Nomino za viumbe

vyenye uhai isipokuwa

mimea.

  1. Nomino zinazotokana

na vitenzi vinavyowataja

watu. Mzee - wazee

Mtoto - watoto

Mfugaji - wafugaji

Mchezaji - wachezaji

  1. -M- 4. -Mi-
  2. Nomino za mimea
  1. Nomino za vitu

zinazoanza na m-

  1. Nomino za matendo

zinazoanza na m- Mti - miti

Mpera - mipera

Mto - mito

Mwiko - miiko

Mchezo - michezo

  1. -Ki
  2. -Vi
  1. Nomino za vitu

zinazoanza na Ki

(umoja) na Vi (wingi)

  1. Nomino za vitu

zinazoanza na ch

(umoja) na vy- (wingi).

  1. Nomino za viumbe

zinazoambishwa na Ki- ya kudunisha

Kiti - viti

Chakula - vyakula

Kitoto - vitoto

  1. -Ji- 8. -Ma-
  2. Nomino zinazoanza

na Ji- (umoja) na ma-

(wingi)

  1. Nomino za sehemu

za mwili wa binadamu

na mti

  1. Nomino za mkopo

Jiwe - mawe

Goti - magoti

Shati - mashati

Maji, mate, maisha...

zenye ma (wingi)

  1. Nomino zenye

kuelezea dhana ya wingi

japokuwa hazihesabiki. 9. -N- 10.

  1. Nomino ambazo

huanza na N

inayofuatwa na

konsonanti, ch, d, g, j, z

na y katika umoja na

wingi.

  1. Nomino zinazoanza

na Mb- au Mv.

  1. Nomino za mkopo

Zingatia: maumbo yote

ya nomino hizi

hayabadiliki kwa umoja

na wingi.

Nguo, nchi, njaa

Mbuga, mboga, mvua

  1. -U- 12. -N-
  2. Nomino zote

zinazoanza na u-umoja

na N wingi. Uso - nyuso

Uzi - nyuzi

  1. -U- 14. -Ma- Nomino zote zinazoanza

na u (umoja) na ma

(wingi). Uasi - maasi

Ugonjwa - magonjwa

  1. -ku- Nomino zinazotokana

na vitenzi zinazoanza na

Ku- (vitenzi jina)

Kusoma

Kucheza

Kuimba

kuruka

  1. PA Huonesha mahali hasa pahala
  2. -Mu- Huonesha mahali pa

ndani

Muhali- 18. -ku- Huonesha mahali pa

mbali au mahali

pakubwa zaidi au hata

mahali popote. Kuhali (kwenu)

Wanaisimu wengine kama Ashton na Broomfield waliainisha nomino baada ya

Meinhof. Walifuata mtindo wa Meinhof isipokuwa waliziweka katika ngeli moja

nomino za umoja na wingi ambazo zinachangia mzizi mmoja baada ya

kuziona kuwa ni tofauti. Kwa uainishaji huu, walipunguza idadi ya ngeli hadi

kufikia 9 tu. Ngeli Mifano ya nomino

  1. Mu/Wa Mtoto - watoto

Mpishi - wapishi

  1. M/Mi Mti - miti

Mwembe - miembe

  1. Ki/Vi Kiti - viti

Kitabu - vitabu

  1. -N- Ngozi, nyota
  2. Ji/Ma Jiwe - mawe

Jino - meno

  1. U/N Uzi - nyuzi

Uso - nyuso

  1. U/Ma Ugonjwa - ugonjwa

Uasi - maasi

  1. Ku

Pa

Mu

Mahali: kule, pale, mle

  1. Ku Kuimba, kucheza, kuoga, kupiga...

Ubora wa kigezo cha kimofolojia/kimapokeo

  1. Inasaidia kuonesha uhusiano uliopo kati ya lugha za kikoa kimoja. Kigezo

hiki kinasaidia kuthibitisha kuwa, Kiswahili ni kibantu. 2. Husaidia kuonesha umoja na wingi katika nomino za kiswahili. Kwa mfano:

mtoto - watoto. Udhaifu wa kigezo cha kimofolojia

  1. Baadhi ya nomino huwa na viambishi vya umoja na wingi ambavyo ni

tofauti na viambishi vinavyoitambulisha ngeli hiyo.

Mfano

Ki-Vi

Chakula - vyakula

Ji-Ma

Jambo - mambo

Ngeli hizo hapo juu, mianzo yake ni tofauti na kitambulisho cha ngeli. 2. Baadhi ya nomino hazina viambishi vyovyote

Nomino hizi hazipaswi kuingizwa katika kundi lolote, lakini ziliingizwa katika

ngeli fulani fulani. Kwa mfano nomino za kigeni ambazo hazina viambishi ziliingizwa katika ngeli

ya N-, sahani, baiskeli, eroplane n.k. 3. Kuna viambishi vinavyofanana

Kwa mfano, ngeli ya kwanza inawakilishwa na kiambishi Mu-, kiambishi hiki

kinajitokeza vilevile katika ngeli ya 3 na 17. Hali kadhalika vile vya ngeli ya 9

na 10,vyote vinawakilishwa na kiambishi N-. Nazo ngeli za 11 na 13

zinawakilishwa na kiambishi U-. Kigezo cha kisintaksia/ Upatanisho wa kisarufi

Huu ni mtazamo wa kisasa wa uainishaji wa ngeli ambao umezigawa nomino

katika makundi kulingana na upatanisho wa kisarufi kati ya nomino na

viambishi awali vilivyo katika vitenzi, yaani vipatanishi. Ngeli katika kigezo hiki ni hizi zifuatazo:

  1. YU/A-WA

Mtu anatembea - watu wanatembea

Mtoto yu aja - watoto wanakuja

  1. U-I

Mti umekauka - miti imekauka

  1. LI-YA

Ua limenyauka - maua yamenyauka

  1. KI-VI

Kitabu kimechanika - vitabu vimechanika

  1. I-ZI

Nguo imechanika - nguo zimechanika

  1. U-ZI

Uzi umekatika - nyuzi zimekatika

  1. U-YA

Ugonjwa umeenea - magonjwa yameenea

  1. KU- Kuimba kunafurahisha
  2. PA/MU/KU

Mahali pale panafaa

Mahali mle mnafaa

Mahali huku kunafaa

Faida za kigezo cha kisintaksia

  1. Kila nomino ina kipatanishi katika kitenzi
  2. Mwainisho wa upatanisho wa kisarufi hautatanishi kwa kuwa kiambishi

awali huwa bayana sana kama kinarejelea kiumbe chenye uhai, kisicho na

uhai au hali. Kwa mfano: ameanguka (mtu, mnyama) umeanguka (ukuta, mti, unyayo)

Matatizo ya kigezo hiki

  1. Kuna vipatanishi vinafanana katika ngeli hizi. Kwa mfano, ngeli ya 2, 6, na 7

katika umoja zote zinawakilishwa na kiambishi cha ngeli u- 2. Katika ngeli ya kwanza, kipatanishi cha umoja YU ni cha kilahaja zaidi na

siyo Kiswahili sanifu. Kwa mfano, mtoto yu aja. 3. Huziweka nomino za maumbo tofauti katika ngeli moja. Kwa mfano: mtu, ndege, ng’ombe, mdudu n.k

Matumizi ya Orejeshi

Orejeshi ni kiambishi kinachotumiwa kurejelea kwenye nomino ambayo huwa

imetajwa kabla ya kitenzi chenyewe kutajwa. Kwa mfano

Uliyemtaka amelala.

Walichokula ni wali maharage

Utokeaji wa umbo la orejeshi katika ngeli za nomino

Umbo la orejeshi huweza kutokea katika mazingira haya

  1. Katikati

Mtoto aliyekuja jana amelala sokoni. Kisu kilichonunuliwa ni butu sana. 2. Mwishoni

Jino liumalo hutolewa. Chui akimbiaye ni mwoga. Mtoto asomaye hufaulu. 3. Orejeshi inayopachikwa kwenye mzizi wa amba- Kitabu ambacho umesoma kimechanika

Juma amepewa adhabu ambayo itamtesa sana. Mtoto ambaye atafaulu atapewa zawadi. Dhima za umbo la orejeshi katika tungo za Kiswahili

  1. Hutumika kama kirejeshi

O rejeshi hurejelea kwa mtendwa au mtenda. Kwa mfano

Wazee waliolala. 2. Hudokeza mahali

Hudokeza mahali ambapo kitendo kimefanyika. Vidokezo vya mahali ni: po, ko

na mo. Kwa mfano

Alipokaa ni pabaya. Alikoenda hapajulikani. Alimolala mna maajabu. Po hudokeza mahali dhahiri.

Ko hudokeza mahali pasipo dhahiri. Mo hudokeza mahali ambapo ni ndani ya kitu. 3. Hudokeza wakati

Hudokeza wakati kitendo kilipofanyika. Kwa mfano: - Tulipotoka walifunga mlango. - Utakapomuona umpige risasi. 4. Hutumika kama kiunganishi

O rejeshi hutumiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi

kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano. Kwa mfano

Mtoto aliyekuja jana ameondoka. Ye imetumika kuunga sentensi, mtoto amekuja na mtoto ameondoka. 5. Hudokeza namna

Hudokeza namna au jinsi kitendo kilivyofanyika ama mtu au kiitu kilivyo na

huundwa na kirejeshi -vyo-. Kwa mfano

Anavyocheza anafurahisha watazamaji. Anavyovaa anachukiza walimu. Makosa ya Kisarufi na Kimantiki Katika Lugha

Watumiaji wa lugha hufanya makosa mbalimbali watumiapo lugha. Ni jambo

lisilowezekana kukosa makosa katika lugha fulani. Makosa ya kisarufi

Makosa haya huangazia matamshi, maumbo na miundo ya tungo. Makosa ya

kisarufi yanajumuisha

  1. Makosa ya msamiati

Katika kipindi cha mazungumzo, wazungumzaji huchanganya msamiati kama

inavyooneshwa katika mfano

Kuchanganya neno ‘nona’ na ‘nenepa’

Kwa mfano: siku hizi umenona sana. Hii siyo sahihi kwa sababu mtu husemwa

amenenepa na mnyama ndiye hunona. Kuchanganya neno ‘mazingira’ na ‘mazingara.’ Makosa ya kimsamiati yanasababishwa na: - mzungumzaji kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa lugha anayotumia. - utani miongoni mwa watu. 2. Makosa ya kimuundo

Haya ni makosa ambayo hutokea katika muundo wa sentensi za kiswahili. Kwa kawaida sentensi huanza na nomino na huwa na vitenzi. Kwa mfano:

Paka mweusi amemkamata panya kwa haraka. Kosa la kimuundo linakuwa: mweusi paka amemkamata panya kwa haraka. Pia, kuna makosa katika upatanisho wa kisarufi. Kwa mfano:

Ni makosa kusema, ‘sikuwa ninajua kuwa Tunu ni dada yako.’ sahihi ni,

‘sikujua kuwa Tunu ni dada yako.’ Sisi sote tunapenda nyama - sisi wote tunapenda nyama. Kalamu yangu imeibiwa - kalamu yangu imeibwa. Nimekuja hapa ili kusudi niongee na ninyi - nimekuja hapa kusudi niongee na

ninyi. 3. Makosa ya matamshi

Wakati mwingine watu hushindwa kutamka maneno ya Kiswahili au

huchanganya na kubadili sauti za lugha. Mifano: wakurya hutumia r badala ya l. Mimi ninaenda kurara badala ya kulala. Wandali (Ileje) hutumia s badala ya z, dh na th. Selasini badala ya thelathini. Sahabu badala ya dhahabu. Wapare hutumia ‘th’ badala ya ‘s’. thatha nakuelewa. Badala ya sasa. Wanyakyusa hutumia ‘f’ badala ya ‘v’. hifi ni fiatu fyangu. Badala ya hivi ni viatu

vyangu. Makosa ya matamshi husababishwa na athari ya lugha mama.

  1. Kosa la kuongeza vitamkwa

Baadhi ya wazungumzaji huongeza vitamkwa mahali visipotakiwa. Mifano

Amekwendaga kwao. Badala ya amekwenda kwao. Mtoto msafi. Badala ya mtoto safi. 5. Kosa la kuacha maneno

Wazungumzaji wengine huacha maneno katika sentensi. Damasi ameondoka kazini. Mzungumzaji anakusudia kusema Damasi

ameondoka kwenda kazini. 6. Makosa ya tafsiri sisisi

Haya ni makosa yanayofanywa na mtu pale anapotafisiri neno kwa neno. Mfano, neno la kiingereza wash out likitafsiriwa vibaya linaweza kuleta

sentensi kama hii. Nyumba zimeoshwa na mvua. Kosa jingine ni kutumia aidha...au. Wakati huu aidha yuko mjini au kazini. Sahihi ni wakati huu yuko ama kazini au mjini. Kosa hili limesababishwa na

tafsiri sisisi ya neno la kiingereza, neither...nor. Makosa ya Kimantiki

Haya ni makosa ambayo yamekosa mtiririko wa fikra zilizopangwa ili kujenga

hoja yenye kukubalika. Mifano

Usimwage kuku kwenye mchele mwingi badala ya usimwage mchele kwenye

kuku wengi. Gari imeingia chui badala ya chui ameingia ndani ya gari.

Ili kuondoa makosa yanayotokea katika lugha, ni vyema msisitizo ukawekwa

shuleni ili wanafunzi wazoee kuzungumza lugha sahihi. Pia, changamoto kubwa ipo katika vyombo vya habari. Watangazaji wengi

wamekuwa wakitangaza kwa kuchanganya kiswahili na kiiingereza, hii ni

hatari kubwa kwa sababu hata katika vyombo vya habari vya serikali

watangazaji wanafanya makosa ya kuchanganya Kiswahili na kiingereza. Ni

vyema sheria kali zitungwe ili kuweza kunusuru lugha ya Kiswahili. Aina za tungo

Tungo ni matokeo ya kupanga pamoja vipashio sahili ili kujenga kipashio

kikubwa zaidi.

Aina za tungo ni

Neno

Neno ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa na kuandikwa na

zinaleta maana. Mfano, mama. Kirai

Ni tungo yenye neno moja au zaidi lakini haina muundo wa kiima na kiarifu. Mfano, mtoto yule. Kishazi

Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha

ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza

kujitegemea chenyewe. Mfano, mbuzi aliyepotea. Sentensi

Sentensi ni tungo yenye kiima na kiarifu na inaleta maana. Mfano, mama

anapika pilau jikoni. Aina za Virai

Kuna aina tano za Virai: - Virai nomino

  • Virai vitenzi - Virai vivumishi - Virai vielezi - Virai viunganishi

Virai nomino

Kirai nomino ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino. Miundo ya Virai nomino

  1. Nomino peke yake. Mfano: chaki, dada, Juma.
  2. Nomino mbili au zaidi. Mfano: Baba na mama.
  3. Nomino na kivumishi kimoja au kadhaa. Mfano: Mtu mnene.
  4. Nomino na sentensi. Mfano: mtoto aliyemletea mama yake kuni jana. V. Nomino, kivumishi na sentensi. Mfano: kijana yule mrefu aliyemnunulia

mwanangu soda jana asubuhi.

  1. Nomino na Kirai kivumishi. Mfano: mzee mwenye duka kubwa kabisa kule

kijijini. Miundo ya virai vitenzi

  1. Kitenzi peke yake. Mfano, amekufa.
  2. Kitenzi na nomino moja. Mfano, amempiga Juma.
  3. Kitenzi na nomino mbili. Mfano, amempa mtoto chakula.
  4. Kitenzi na kitenzi. Mfano, anapenda kusoma. V. Kitenzi na nomino na kitenzi. Mfano, anamfundisha mtoto kusoma. Miundo ya virai vivumishi
  5. Kivumishi na kielezi chake. Mfano, zuri kabisa.
  6. Kivumishi na kirani nomino. Mfano, enye duka kubwa.
  7. Kivumishi na kirai kitenzi. Mfano, enye kupenda mambo makubwa.
  8. Kivumishi na kirai kivumishi. Mfano, mwingine mwenye matatizo. V. Kivumishi na kirai kiunganishi. Mfano, zuri wa kutamanika. Aina za vishazi

Kuna aina mbili za vishazi

  1. Kishazi huru

Hiki ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu. Mfano

Anacheza mpira. 2. Kishazi tegemezi

Hiki ni kishazi ambacho kinatawaliwa na kitenzi kisaidizi. Mfano

Mwalimu aliyefundisha darasani

Aina za vishazi tegemezi

Vishazi tegemezi vivumishi

Hivi ni vishazi ambavyo hufanya kazi ya vivumishi.

Mfano

Samaki aliyepotea jana

Vishazi tegemezi vielezi

Vishazi hivi hufanya kazi ya vielezi katika tungo. Mfano

Kijana alilala aliposemwa

Muundo wa sentensi

Sentensi ina sehemu kuu mbili

Kiima

Ni sehemu katika sentensi inayojaza nafasi ya mtenda au mtendewa wa jambo

linaloelezwa. Mfano

Baba anacheza mpira

Kiarifu

Ni sehemu katika sentensi inayojazwa na maneno yanayoarifu tendo

lililofanywa, linalofanywa na litakalofanywa. Mfano

Juma ni mkulima. Dhima za Vishazi

  1. Kufanya kazi ya kivumishi katika tungo. Mfano, chakula kilichopikwa jana
  2. Kufanya kazi ya vielezi katika tungo. Mfano, mtoto alilia alipopigwa. Uchanganuzi wa sentensi

Uchanganuzi wa sentensi ni kitendo cha kuigawa sentensi katika sehemu

mbalimbali ambazo huunda sentensi hiyo. Hatua muhimu katika uchanganuzi wa sentensi

  1. Taja aina ya sentensi, kama ni sahili, ambatano au changamano.
  2. Taja sehemu zake kuu, yaani kiima na kiarifu. 3. Taja sehemu kuu za kiima na kiarifu au za kirai nomino na kirai kitenzi. 4. Taja aina zote za maneno zilizomo katika sentensi hiyo. 5. Iandike upya sentensi hiyo. Maswali ya uchanganuzi wa sentensi

Tumia maarifa uliyoyapata kidato cha nne, kujibu maswali haya ya

uchanganuzi wa sentensi

  1. Katika sentensi hizi, kila sentensi ichanganue kwa njia ya mishale, matawi, maneno na visanduku:
  2. Zacharia ni mtu mkarimu sana.
  3. Mtoto aliyekimbia shule, amerudi mjini.
  4. Baba anacheza na mama anapika. Uundaji wa maneno

Uundaji wa maneno ni utengenezaji wa maneno mapya katika lugha. Sababu za uundaji wa maneno

  1. Kukuza msamiati kwa ajili ya matumizi ya lugha ya kila siku. 2. Kuweza kutafsiri mengi kutoka lugha yako au ya kigeni. 3. Kupata msamiati utakaokubalika katika shughuli mahususi za kila siku. Mfano: benki, forodhani au jeshini. 4. Kukuza msamiati ili utumike katika masuala ya kitaifa kama utamaduni. Njia mbalimbali za uundaji wa maneno
  2. Kutohoa

Kutohoa ni njia ya kuchukua maneno katika lugha nyingine na kuyaingiza

katika lugha nyingine. Kiswahili kimetohoa neno la kiingereza ‘tractor’ na kuwa

trekta. Neno la kireno bibo. Neno la kijerumani ‘pilao’ na kuwa ‘pilau’ na

maneno mengi kutoka lugha nyingi. 2. Miambatano

Ni njia ya uundaji wa maneno ambayo huunga maneno mawili au zaidi

kutengeneza neno jipya. Mfano

Mwalim

Mwananchi, mchezakwao, mpigamaji, njugumawe n.k

  1. Mpangilio tofauti wa mofimu

Mfano, neno lima likibadilishwa mpangilio, linatoa maneno mengine kama

mali, imla, lami, mila, n.k

  1. Kufananisha sauti, umbo, sura au tabia

Mifano: pikipiki, mtutu, nyau, kifaru, beberu (mtu anayeonea wengine). 5. kufupisha maneno

Kwa mfano, shemeji - shem, Dar es Salaam - Dar, Televisheni - TV, Baraza la

Mitihani la Taifa - BAMITA n.k

  1. Urudufishaji

Mifano: polepole, nungunungu, kiwiliwili, kizunguzungu n.k

  1. Kuambisha viambishi nyambuaji

Mifano, soma - msomi, taifa - taifisha, refu - refusha, haraka - harakisha n.k