Kiswahili · Kidato 5

Maana ya tafsiri

Dakika 14 za kusoma ·

Tafsiri ni kitendo cha kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja

{lugha chanzi} na kuweka badala yake mawazo yanayolingana katika lugha nyingine

{lugha lengwa}. Mfasiri

Mfasiri ni mtu anayefanya tafsiri kutoka lugha moja hadi lugha nyingine. Sifa za mfasiri

  1. Ajue lugha zote mbili
  2. Awe amesoma maandishi ya matini chanzi hadi ayafahamu kinaga ubaga halafu

aweze kuyafikiria katika lugha lengwa. Ø Awe na ufahamu mkamilifu wa ujumbe au mada iliyoandikwa katika matini

chanzi na uwezo au jinsi ya kuelezea ujumbe au mada hiyo kwa ufasaha

katika lugha lengwa. Ø Awe mjuzi wa TEHAMA. Ø Afahamu vizuri watu, jamii na utamaduni wa watumiaji wa lugha chanzi na

lugha lengwa. Ø Afahamiane na watu wengi, yaani kujichanganya changanya na watu wa fani

au sekta mbalimbali. Ø Awe na tabia yakushirikiana na watu wengine katika shughuli za kufasiri. Mambo ya kuzingatia katika tafsiri

  1. Soma matini nzima

hii itasaidia kubaini ni aina gani ya marejeo muhimu yatakayosaidia kutafsiri

mfano wa

marejeo hayo ni kama kamusi, ensiklopedia, orodha ya msamiati na istilahi mpya. 2. Baini lengo la matini chanzi

Kubaini lengo la matini kutakufanya utoe tafsiri safi inayoendana na habari

unayoifasiri. 3. Baini wasomaji lengwa (hadhira)

maswali anayotakiwa kujiuliza mfasiri ili aweze kuibaini hadhira ya matini yake ya tafsiri

ni: je msomaji wa tafsiri yake ni nani? Ana kiwango gani cha elimu, ni msomi wa

kawaida au msomi aliyebobea? Wana umri gani na ni jinsia gani? Je hadhira yake imo

katika tabaka gani katika jamii? Kwa kuibaini hadhira ya matini lengwa itamsaidia

mfasiri kuamua kuirahisisha tafsiri yake au kuifanya iwe ngumu kutegemeana na uwezo

wa hadhira ya tafsiri lengwa. 4. Kubaini mtindo wa matini chanzi

Mfasiri anatakiwa kujua, matini chanzi imetumia mtindo gani katika kuwasilisha maudhui

yake, imetumia mtindo wa kirasimu? Au imetumia mtindo wa kitaaluma? Je imetumia

mtindo wa kiuandishi wa habari au mtindo wa kimawasiliano yasiyo rasmi? Je

ametumia lugha rasmi au ya mtaani? Na inatakiwa mtindo wa matini chanzi ilingane na

ile ya matini lengwa. Tazama mifano ifuatayo

Kingereza: Please, Sir do no mind it! If I arrive earlier, I’ll wait for you

Kiswahili: Mkubwa! Kausha tu! Na kama nitatia maguu mapema, nitakusikilizia Palepale

Ukiangalia mfano huo, utaona kuwa, mitindo iliyotumika katika sentensi hizo ni mitindo

miwili tofauti, katika mfano tuliouangalia katika lugha chanzi, mtindo wa lugha uliotumika

ni mtindo rasmi, wakati katika tafsiri [lugha lengwa] mtindo uliotumika ni mtindo wa

lugha ya mtaani, jambo ambalo si zuri katika tafsiri. Mtindo wa lugha lengwa sharti

ulingane na mtindo wa lugha chanzi. 5. Kusoma matini kwa mara ya mwisho

Mfasiri anashauriwa aisome matini chanzi kwa mara ya mwisho huku akipigia mstari au

kuandika katika kidaftari kidogo msamiati, istilahi na misemo muhimu ya matini chanzi

kama vile, methali, nahau maneno ya kitamaduni yasiyotafsirika, majina maalumu, n.k. kwa kupigia mstari au kuyaandika katika kidaftari kidogo ili iwe rahisi kwa mfasiri

kuyatafutia visawe vyake kabla hata ya kuanza kutafsiri lakini pia kumsaidia mfasiri

asiyasahau wakati wa kutafsiri. Mambo ya kuzingatia wakati wa mchakato wa kutafsiri. 1. Maandalizi ya kutafsiri

Katika hatua hii, mfasiri anatakiwa kufahamu vizuri maudhui ya matini chanzi, ujumbe

wake, mtindo wa matini na kuwekea alama sehemu zenye utata au zisizoeleweka vizuri, anashauriwa kupigia mstari au kuandika katika kidaftari kidogo msamiati, istilahi na

misemo muhimu ya matini chanzi kama vile, methali, nahau maneno ya kitamaduni

yasiyotafsirika, majina maalumu, n.k. kwa kupigia mstari au kuyaandika katika kidaftari

kidogo ili iwe rahisi kwa mfasiri kuyatafutia visawe vyake kabla hata ya kuanza kutafsiri

lakini pia kumsaidia mfasiri asiyasahau wakati wa kutafsiri au kuyatolea ufafanuzi zaidi

katika tafsiri yake. 2. Uchambuzi wa matini chanzi

Katika hatua hii, mfasiri anatakiwa kuchunguza kwa makini maneno, methali, nahau, misemo pamoja na maelezo mengine ya matini chanzi aliyoyaandika au kuyapigia

mstari katika hatua ya maandalizi na kuyatafutia visawe vyake katika lugha lengwa, hapa mfasiri anashauriwa kutumia marejeo mbalimbali kama vile, kamusi, ensiklopedia, orodha ya msamiati na istilahi mpya. 3. Uhawilishaji

Uhawilishaji ni uhamishaji wa mawazo kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa, au

uhamishaji wa mawazo au ujumbe kutoka matini asilia kwenda matini ya tafsiri. Hii ina

maana kuwa katika hatua hii, visawe vya kisemantiki [kimaana] vya matini chanzi

vilivyobainishwa katika hatua ya uchambuzi huamishwa katika matini lengwa [kutoka

lugha chanzi kwenda lugha lengwa] na kupangwa vizuri kisarufi na kimantiki ili fasiri

hiyo iwe na maana kwa wasomaji wake. 4. Kusawidi /Kuandaa rasimu ya kwanza ya tafsiri. Katika hatua hii, mfasiri huandika rasimu yake ya kwanza ili kupata picha fulani ya

matini aliyoikusudia, katika uandaaji wa rasimu ya kwanza, kwa kufanya hivi, mfasiri

anaweza kugundua kuwa anahitaji taarifa zaidi tofauti na alizozipata katika hatua ya

uchambuzi, na hivyo kulazimika kuchunguza zaidi matini chanzi na hata kupekua zaidi

na zaidi marejeo yake aliyoyaandaa kwa kuyatumia katika tafsiri. Jambo la kuzingatia, mfasiri anatakiwa wakati akihamisha mawazo au ujumbe azingatie umbo na lengo la

matini chanzi ili kutoathiri tafsiri yake. 5. Kudurusu / kuipitia rasimu ya kwanza

Baada ya kusawidi rasimu ya kwanza, mfasiri anatakiwa kuivundika rasimu yake ya

tafsiri kati ya juma moja hadi mawili baada ya kukamilika kwake na kuanza kuidurusu/

kuipitia rasimu hiyo kwa jicho la kihakiki zaidi na kuangalia kama kuna makosa ambayo

yamejitokeza katika rasimu yake au la na kuyafanyia marekebisho pale inapobidi. 6. Kusomwa kwa rasimu ya tafsiri na mtu/watu wengine

Wasomaji hao wanaweza wakahakiki,wakashauri, n.k. Wasomaji hawa husaidia kuona

kama tafsiri iko sahihi, inaeleweka na ina mtiririko mzuri wenye mantiki.

  1. Usawidi /Kuandika rasimu ya mwisho

Baada ya kupata maoni kutoka kwa wasomaji wa pili, mfasiri anaweza kuyatumia maoni, mapendekezo na maelekezo yao kusahihisha tena tafsiri yake na hatimaye kuandaa na

kutoa rasimu ya mwisho ambayo itakuwa tayari kwa kusomwa na wasomaji. Njia / mbinu za Tafsiri

Zipo njia mbalimbali ambazo hutumika katika kutafsiri, baadhi ya njia hizo ni kama vile

(i) Tafsiri ya neno kwa neno. (ii) Tafsiri sisisi. (iii) Tafsiri ya kimaana/uwazi

(iv) Tafsiri ya kimawasiliano. (i) Tafsiri ya neno kwa neno

Hii ni aina ya tafsiri ambayo mofimu na maneno hufasiriwa yakiwa pweke pweke kwa

kuzingatia maana zake za msingi bila kujali muktadha. Katika aina hii ya tafsiri

mpangilio wa mofimu na maneno wa lugha chanzi hubakia vilevile bila kubadilika. Na

kwa kawaida matini inayotafsiriwa huandikwa chini ya matini ya lugha chanzi. Tazama

mifano ifuatayo ya tafsiri ya neno kwa neno

Kiswahili: Alisoma hadi asubuhi

Kingereza: He/past/study/until/morning

(ii) Tafsiri sisisi

Hii ni aina ya tafsiri ambayo maneno hufasiriwa yakiwa pweke pweke kwa kuzingatia

maana za msingi katika lugha chanzi bila kujali sana muktadha lakini ni tafsiri

inayofuata mfumo wa kisarufi hasa kipengele cha kisintaksia ya lugha lengwa. Ebu

tuangalie mifano ifuatayo

Kingereza: He was taken at the Central Police Station

Kiswahili: Alipelekwa kwenye kituo cha kati cha police. (iii) Tafsiri ya kisemantiki/maana au uwazi [Semantic Translation]

Hii ni aina ya tafsiri ambayo mfasiri huegemea zaidi kwenye lugha chanzi. Katika aina

hii ya tafsiri, mfasiri hufasiri kila neno katika sentensi jinsi lilivyo lakini kwa kufuata sarufi

hususani vipengele vya kisemantiki na kisintaksia ya lugha chanzi. Inaitwa tafsiri ya

kisemantiki kwa sababu, mfasiri anapofasiri hutakiwa kuweka mkazo kwenye maana ya

matini kama ilivyokusudiwa na mwandishi wa matini chanzi.

Kiswahili: Alikwenda mpaka hospitali

Kingereza: He went up to hospital

Aina hii ya tafsiri, ina faida kubwa katika ukuaji wa lugha lengwa kwa kuingiza miundo

ya misemo kutoka lugha chanzi, mathalani, lugha ya Kiswahili imepokea miundo mipya

ya misemo kutoka lugha ya Kingereza, baadhi ya miundo hiyo ni kama vile

Kiswahili: Usiku mwema kutoka Kingereza: Good night

Kiswhili: Mabibi na mabwana kutoka Kingereza: ladies and gentlemen

  1. Tafsiri ya kimawasiliano/ huru

Hii ni aina ya tafsiri inayomlenga msomaji [hadhira] wa matini lengwa, ambaye katika

aina hii ya tafsiri hatarajii kukutana na ugumu wowote katika matini atakayoisoma, bali

hutarajia kukutana na tafsiri nyepesi ya dhana za kigeni katika utamaduni na lugha yake

kwa kadiri itakavyoonekana. Hivyo basi, mfasiri wa aina hii ya tafsiri yuko huru kutafuta

maneno na mafungu ya maneno yanayolingana na maneno, methali, nahau, utamaduni

na mazingira ya lugha lengwa, pamoja na kuwa tafsiri ya kimawasiliano kufuata sarufi

ya lugha lengwa ni lazima pia ifuate utamaduni, mazingira na historia ya jamii ya lugha

lengwa. Tuangalie mifano ifuatayo

Kingereza: Jane married John

Kiswahili: John alimwoa Jane

Kingereza: No need to cry over spilt milk

Kiswahili: Maji yakimwagika hayazoleki

Hivyo basi, katika aina hii ya tafsiri, mfasiri hutafuta methali au misemo inayopatikana

katika lugha lengwa inayohusiana au kukaribiana na ile ya lugha chanzi. Ebu jaribu

kutafsiri misemo/methali zifuatayo ya lugha ya Kiswahili kwenda lugha ya Kiingereza

Adhabu ya kaburi aijuaye maiti

Asiyekubali kushindwa si mshindani

Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa

Ukalimani ni nini?

Ukalimani umefasiliwa kuwa ni, uhusishaji wa kuhamisha maana kutoka lugha moja

(lugha chanzi) kwenda lugha nyingine (lugha lengwa) katika mazungumzo. Hivyo basi

tunaweza kusema pia, ukalimani ni hali ya mtu kuhamisha mawazo ya

kinachozungumzwa kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine katika mazungumzo. Hii

ina maana kuwa ukalimani ni lazima uhusishe pande mbili, upande wa kwanza sharti

awepo mtu anayezungumza lugha fulani na upande mwingine kunakuwa na mtu

ambaye anasikiliza hicho kinachozungumzwa na kuyarudia hayo yanayozungumzwa

kwa kutumia lugha nyingine tofauti na ile iliyotumiwa na mazungumzaji wa kwanza. Sifa za mkalimani bora

  1. Awe mtu anayezielewa lugha chanzi na lugha lengwa vizuri
  2. Awe ni mtu ambaye ameishi pande zote za lugha anazozikalimani ili kuelewa

mila na desturi za watumiaji wa lugha hizo. 3. Awe stadi wa ukalimani, hapa inatakiwa awe na uhodari wa kukalimani, kuzungumza vizuri, maneno kusikika, awe na uwezo wa kukalimani neno kwa

neno au sentensi na sentensi, kutumia ishara zinazoambatana na ishara za

mzungumzaji wa lugha chanzi na hata kutumia mtindo anaodhani unaweza

kuwavutia wasikilizaji wake. 4. Muadirifu, ambaye hawezi kupotosha au kubadili ukweli wa kinachozungumzwa, nahii ni muhimu kwa sababu wakalimani hutumika hadi mahakami hivyo kama si

mwadirifu huweza kuufanya upande mmoja ukakosa haki inayostahiri. 5. Asiwe mbaguzi, hapa ina maana mkalimani asiamue kupotosha ukweli wa kile

kinachozungumzwa kwa kuwa tu kinaendana kinyume na itikadi yake ya kisiasa, kidini, kiutamaduni, n.k. wala asiangalie jinsia ya mtu umri au hali ya mtu

anayemfanyia ukalimani. Mambo ya kuzingatia katika Ukalimani

Kwa ujumla yapo mambo kadha wa kadha, ambayo mkalimani anatakiwa kuyazingatia

anapotaka kufanya ukalimani, mambo hayo tunaweza kuyagawa katika makundi mawili, ambayo ni:

  1. Kabla ya kuanza ukalimani

Katika hatua hii, mkalimani anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo

(a) Awe na uelewa mzuri wa lugha zote anazotaka kukalimani, hapa tuna maana

kuwa awe na uwezo wa kuzungumza na kuelewa lugha chanzi na lugha

lengwa, hii itasaidia mkalimani kutopotosha kile kinachozungumzwa na

mzungumzaji wa lugha chanzi. (b) Awe anaijua historia na utamaduni wa jamii zote mbili, yaani ile ya lugha

chanzi na ile ya lugha lengwa. (c) Kama ni ukalimani rasmi, ni vizuri kwa mkalimani akamjua mzungumzaji wa

lugha chanzi, ni vema pia ukafanya naye mazungumzo kidogo ili kumzoea, na kutambua vionjo vyake ili iwe rahisi kwa mkalimani pindi atakapokuwa

anafanya ukalimani asionekane kama mgeni.

(d) Vilevile ni muhimu kwa mtu anayekalimani, akawa na uelewa mzuri wa mada

inayozungumzwa, hii itamrahisishia mkalimani katika ukalimani wake. 2. Katika ukalimani wenyewe

Mkalamani anapokuwa amesimama mbele ya hadhira [wasikilizaji] pamoja na

mzungumzaji wa lugha chanzi kwa ajili ya kuanza ukalimani, anatakiwa

kuzingatia mambo yafuatayo

(a) Kuwa makini katika kusikiliza kile kinachozungumzwa na mzungumzaji wa

lugha chanzi ili kuepuka kuachwa mahali na kuepuka kumuomba

mzungumzaji kurudia mara kwa mara. (b) Itambue hadhira ya lugha lengwa, ni watu wa namna gani, wana kiwango

gani cha elimu, ni wasomi wa kawaida au waliobobea, ni watu wa jinsia na

umri gani,? Hii itakusaidi kujua aina ya msamiati na miundo ya tungo

utakayoitumia, kama iwe rahisi au migumu kutokana na hadhira yako ilivyo. (c) Tumia mitindo unayodhani itaeleweka vema na hadhira/ wasikilizaji wa lugha

lengwa, kwa mfano kama hadhira yako ni vijana, jaribu kutumia mitindo

inayopendwa na vijana, kama wasikilizaji wako ni watu rasmi na we huna

budi kuwa rasmi. (d) Weka mkazo sehemu ambazo mzungumzaji wa lugha chanzi anaweka

mkazo ili kuepuka utofauti yako na mzungumzaji wa lugha chanzi, na hata

kuepuka kuathiri lengo la mzungumzaji wa lugha chanzi. (e) Unatakiwa pia kutumia ishara zinazotumiwa na mzungumzaji wa lugha chanzi, hii itawafanya wasikilizaji waamini kile kinachozungumzwa na mzungumzaji

wa lugha chanzi ndiyo kilekile kinachozungumzwa na mkalimani. (f) Usiwe muda mwingi unamtazama mzungumzaji wa lugha chanzi na

kusahahu kuitazama hadhira yako, hivyo unatakiwa kuitazama hadhira yako

ili kugundua kama wako pamoja na wewe au kuna sehemu hawajakuelewa ili

uweze kuwafafanulia zaidi. (g) Muombe mzungumzaji wa lugha chanzi kurudia sehemu unayodhani

hujaisikia au hujaielewa vizuri, kwani ni makosa kwa mkalimani kukalimani

sehemu au jambo ambalo hukulisikia vizuri au kulielewa. Dhima za Tafsiri na Ukalimani

  1. Hutuwezesha kujifunza lugha tofauti. 2. Hutumika kama njia ya mawasiliano. 3. Tafsiri na Ukalimani hutumika kueneza utamaduni. 4. Tafsiri na Ukalimani ina dhima ya kuwasilisha ujumbe wa manufaa kwa

watu ambao hawafahamu lugha chanzi [lugha asilia]

Changamoto/ mapungufu katika tafsiri na Ukalimani

  1. Tofauti za kiisimu kati ya lugha chanzi na lugha lengwa.

Tofauti za maumbo, miundo na maana kati ya lugha ya Kiswahili na lugha ya Kingereza

wakati mwingine husababisha matatizo au upungufu katika tafsiri na ukalimani. Kwa mfano

maumbo ya vitenzi vya Kiingereza huruhusu kauli nyingi elekezi kutoonesha umoja au wingi

wa wahusika wala majina ya vitu mahususi vinavyoambatana na maelekezo yanayotolewa

tofauti maumbo ya vitenzi vya Kiswahili ambavyo huonesha umoja na wingi wa wahusika na

hata kuwa na majina ya vitu husika, tazama mifano ifuatayo kama ilivyotolewa na, Mwansoko

[2006]

Kingereza Kiswahili

No parking - Usiegeshe gari hapa [je kisichoruhusiwa kuegeshwa ni gari tu?

Vilevile tofauti za maana kati ya lugha ya Kingereza na Kiswahili huweza kuathiri tafsiri au

ukalimani, mathalani

Kiswahili Kingereza

Wasiojiweza - Disabled [Siyo wote wasiojiweza ni walemavu]

[na siyo walemavu wote hawajiwezi]

(ii) Tofauti za mitindo kati ya lugha chanzi na lugha lengwa

Tofauti za mitindo ya uzungumzaji pia, huweza kuathiri tafsiri na ukalimani na hii ni kwa

sababu unaweza kukuta kuna mitindo fulani inaweza kutumika katika muktadha fulani lakini

ikishindwa kupata tafsiri katika lugha nyingine katika muktadha ule ule.mathalani

Kingereza: Kiswahili

(i) Thou shall not steal [mtindo wa kidini] ? Usiibe

Do not steal [mtindo wa kawaida] ? Usiibe

(ii) Lend me your ears [mtindo wa kishairi] ? Naomba mnisikilize

May I have your attention [kawaida] ? Naomba mnisikilize

Tafsiri zote tulizoziangalia katika mfano wa (i) na (ii) zimetoa maana au taarifa ili ile iliyomo

katika matini chanzi lakini tafsiri hizo hazikuzingatia mtindo wa lugha iliyotumika katika matini

chanzi. (iii) Tofauti za kitamaduni kati ya lugha chanzi na lugha lengwa

Tofauti za kiutamaduni, yaani taofauti za kimila, desturi na mazingira ya watumiaji wa lugha

chanzi na lugha lengwa huweza kufanya tafsiri au ukalimani kuwa mgumu, kwa mfano, katika

utamaduni wa Waingereza wana milo minne wakati Waswahili wana milo mitatu na hii

hupelekea kuwa vigumu kupata dhana za milo ya hiyo ya Waingereza katika dhana ya

Kiswahili. Mfano

Waingereza wana: Waswahili wana

Breakfast ------------------ Kifungua kinywa

Lunch ........................ Chakula cha mchana

High tea ........................?

Dinner ........................Chakula cha jioni

Supper .........................?

Kwa hiyo ukiangalia mifano hiyo, utaona kuwa, high tea na supper kuzipata dhana zake katika lugha ya

Kiswahili ni ngumu kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kuwa na milo kama hiyo kwa siku. Lakini pia

inakuwa vigumu kupata tafsiri ya vyakula kama vile ugali, makande katika lugha ya Kiingereza kutokana

na kutokuwa na vyakula vya aina hiyo. (iv) Tofauti za kiitikadi kati ya lugha chanzi na lugha lengwa

Tofauti za kiitikadi pia huweza kuathiri tafsiri na ukalimani, na hii ni kwa sababu, utakuta wafasiri wengi

hususani waandishi wa habari kuegemea katika itikadi zaidi, kwa mfano

Kingereza Kiswahili

Bussnessman ? mlanguzi [tafsiri hii inatokana mfasiri kuathiriwa na itikadi ya ujamaa]

mfanyabiashara [tafsiri hii inatokana mfasiri kuathiriwa na

itikadi ya ubepari]

Freedom fighter ? wapigania uhuru [Tafsiri ya vyombo vya habari vya

Tanzania wakati wa kupigania uhuru]

Magaidi [Tafsiri ya idhaa ya BBC na Radio za AfrikaKusini wakati huo]

Hivyo basi kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, ukalimani mzuri unawezekana kwa kiwango

ambacho mila na desturi zote yaana za lugha chanzi na lugha lengwa zinalingana ama kushabihiana. Na kutokana na umuhimu wa taaluma hii ya tafsiri na ukalimani, serikali kupitia Baraza la Kiswahili la

Taifa Bakita [BAKITA] imeanzisha idara maalumu ya Tafsiri na Ukalimani, na idara hiyo ina majukumu

yafuatayo

Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha mbalimbali kwa masharika, idara, wizara, balozi na watu

binafsi. Kuratibu na kutoa huduma za ukalimani kwenye mikutano ya kitaifa na kimataifa na katika shughuli za

masharika, makampuni na watu binafsi. Kupitia na kuthibitisha tafsiri zilizofanywa na asasi mbalimbali au wafasiri wa nje. Kutoa ushauri kuhusu masula ya tafsiri na ukalimani